Videi
vixen maarufu Agnes Gerald maarufu kama Masogange amefunguka na kuweka
wazi kuwa hivi sasa hataki kabisa masuala ya shobo na watu baada ya kesi
yake badala yake anataka kuwa kivyake.
Wiki
iliyopita Masogange aliponea chupu chupu kwenda jela baada ya
kuhukumiwa miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 ambayo
alifanikiwa kuilipa na kuepuka jela.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Masogange alisema kuwa, kwa
sasa anataka aishi maisha yake ya kawaida na wala hataki kujihusisha na
mambo ya kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo maana anaona
hayo ndiyo yaliyomu-ingiza kwenye misukosuko.
"Sasa
hivi nataka kuishi maisha yangu ya kawaida kabisa, sitaki tena
kujihusisha na mambo ya mitandao, nataka maisha yangu yawe ya kawaida
kabisa“.
Agnes
alikamatwa mwaka jana Kwa Tuhuma za kujihusisha na matumizi ya madawa
ya kulevya na mkemia mkuu wa serikali alithibitisha hayo baada ya
kumpima.


0 comments:
Chapisha Maoni