Msanii
mkubwa Tanzania wa Muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platnumz’, amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema kuwa
anavaa msalaba ambao hauendani na imani yake lakini ukweli unabaki kuwa
siri ya msalaba huo anaijua yeye na kwamba kwake yeye ule sio msalaba
bali ni alama ya kumjumlisha ambayo kwake ina maana sana.
Diamond
amesema hayo kwa sababu kuna kipindi aliwahi kuongelewa hadi na
viongozi wa dini kuwa amekuwa haeleweki kwa sababu anavaa misalaba
ambayo ni kunyume na imani ya dini yake ya kiislamu.
“Cheni
ninayovaa na watu kunidisi kwamba ni msalaba kiukweli huwa ninashangaa
sana kwa maana watu huzungumza kile ambacho hawakifahamu. Kwangu huo si
msalaba, bali ni alama ya jumlisha ambayo ninaona haina tatizo lolote,
kwani alama hiyo inamaana kubwa kwangu ambayo itabaki kuwa siri
yangu!”Aliongea Dimaond akichonga na kipindi cha Mikito Nusu Nusu cha
GPL
0 comments:
Chapisha Maoni