Mbunge
wa Jimbo la Kondoa Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Ediwn Sanda amesema kuwa safu ya uongozi wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kwenye jimbo hilo wamehamia CCM kutokana na kazi
nzuri anazozifanya Rais Dkt. Magufuli
Ameyasema
hayo leo April 27, 2018 alipopata nafasi ya kuwasalimu viongozi
mbalimbali akiwemo Rais Dkt. Magufuli kwenye sherehe za ufunguzi wa
barabara ya Kondoa, Babati yenye urefu wa kilomita 251
“Rais
safu ya uongozi mzima ya CHADEMA imehamia CCM, Mwenyekiti wa Jimbo,
Katibu wa Jimbo, na viongozi wengine kwa uchache wao, kwa kweli
nashukuru sana ila tunakwenda kubomoa moja kwa moja dhana ya upinzani
Kondoa kwani viongozi wao wote wamehamia CCM tayari kutokana na kazi
ambazo unafanya,”amesema Sanda
Baadhi
ya viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakihama kutoka katika
vyama vyao vya siasa na kujiunga na chama tawala Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kwa kile wanachodai kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe
Magufuli.
0 comments:
Chapisha Maoni