Wadau wa tasnia ya filamu na familia ya marehemu Steven Kanumba, leo wanaadhimisha miaka sita tangu kufa kwa msaanii huyo.
Mama yake Flora Mtegoa, amesema yeye kwake msiba huo bado upo kila siku na kudai kila nafsi itaonja mauti.
Mtegoa
ameyasema hayo leo Aprili 7 katika makaburi ya Kinondoni ambapo
walifanya ibada fupi kwa ajili kumbukumbu hiyo akiwa na baadhi ya
wasanii hususani wa kikundi cha Soweto ambao ndio wameisimamia shughuli
hiyo kwa mwaka huu.
Amesema
pamoja na kujitokeza kwa wasanii wachache ambao waliwahi kufaya kazi na
mtoto wake enzi za uhai wake anaamini ni kutokana na wao kuona
wameshamaliza msiba, lakini kwake upo kila siku na kamwe hauwezi
kufutika mpaka mwisho wa uhai wake.
"Ni
kweli idadi ya wasanii maarufu waliokuja hapa ni wachache ukilinganisha
na namna Kanumba alivyoishi nao, lakini ndio hivyo huwezi kuwalazimisha
na isitoshe wao labda wanaona wamemaliza msiba lakini kwangu bado upo
ila ninachowaombea yasije yakawakuta kama haya ndio watajua nini
namaanisha,’’ amesema Mama Kanumba.
Wito wake kwa wasanii Mama Kanumba amewashauri kuwa na upendo kauli ambayo Kanumba alikuwa anapenda kuisema enzi za uhai wake.


0 comments:
Chapisha Maoni