Ikiwa leo April 19, 2018 msanii Alikiba ameoa, mshindani wake kimuziki Diamond Platnumz hajakaa kimya kwenye hilo.
Diamond
amefunguka kuwa amepewa taarifa za Alikiba kuoa siku ya leo, hivyo
amemtumia salamu na kumtakia maisha mema ya ndoa. Kupitia ukurasa wake
wa Intagram tumegulia kile alichogusia kuhusiana na ndoa ya Alikiba;
"Ni
Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata
kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round
hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam
zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka
tele...🔥🔥🔥 " ameandika Diamond.
Msanii Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake Aminah Rekish mjini Mombasa nchini Kenya.


0 comments:
Chapisha Maoni