Ndoa
ya Irene Uwoya na Dogo Janja inazidi kugonga vichwa vya habari, safari
hii msanii Msamii aliyekuwa mpenzi wa Irene hapo awali anatajwa sana
katika ndoa hiyo.
Msanii
na Irene wameacha maswali mengi baada ya hivi karibuni kuanza kusifiana
katika mitandao kitu ambacho baadhi ya watu wanadai hakileti picha
nzuri katika ndoa ya Irene na Dogo Janja.
Sasa
muimbaji huyo akizungumza na E-Newz, EATV amesema yeye amejua na Irene
kwa kipindi kirefu hivyo hata kama mrembo huyo amejuana na mtu mwingine
si sababu ya wao kushindwa kuendelea kuwa marafiki.
“Naichukulia
kawaida sana, nikikujua leo baada ya miaka mitano mbele ukajuana na mtu
mwingine, mkawa na maisha mengine mimi nakujua wewe huyo mtu mwingine
simjui,” amesema.
“Kwa
hiyo ni vitu ambavyo haviwezi kupotea tu, kwanini nianze kupotezea
kwamba yule sasa hivi yupo na fulani sitakiwi kuongea naye, maisha
hayako hivyo” ameongeza.
Hata hivyo ameonya kuwa Irene siyo mke wake na anatambua kuwa ni mke wa mtu.
0 comments:
Chapisha Maoni