Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawatumikie wananchi
kwa uweledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati
akizungumza na watumishi wa wilaya za Masasi na Nanyumbu kwa nyakati
tofauti.
Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi aliwasisitiza watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Alisema
Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie
wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa
mazoea.
“Watumishi
wa umma lazima mtambue kwamba msimamo wa Serikali ni kuwahudumia
wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kiitikadi na kipato.”
Waziri
Mkuu alisema ni vyema watumishi hao kuanza kujitathmini kwa sababu
Serikali haitowavumilia watumishi watakaoshindwa kuwajibika kwa
wananchi.
Pia
aliwataka watendaji hao kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha
iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika
kama zilivyoelekezwa.
Waziri
Mkuu aliwaagiza watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi
kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 27, 2018.
0 comments:
Chapisha Maoni