WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa
kike na ndiyo maana tunawataka watoe taarifa za watu wanaotaka
kuwakwamisha kimasomo kwa watendaji wa vijiji kwenye maeneo yao.
Alitoa
agizo hilo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza kwa
nyakati tofauti na wakazi wa wilaya ya Masasi akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.
Waziri
Mkuu alisema watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii kwa
kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wa aina yoyote na
atakayebainika kukatisha masomo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema
Serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu
atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na
hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya wageni.
“Tukikukuta
na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia
hatua za kisheria. Ole wenu vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti
wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela.”
Waziri
Mkuu alisema kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao
bado wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto kwenda
kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.
Pia
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wote kusoma kwa
bidii ili watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa sababu
watashindwa kufikia masomo yao.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 27, 2018.
0 comments:
Chapisha Maoni