Rais
wa Marekani, Donald Trump amemjibu rapa Jay Z kwa kile alichokisema
kwenye mahojiano na CNN kuhusu matamshi ya kibaguzi yanayodaiwa kutolewa
na kiongozi huyo.
Akizungumza
katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha The Van Jones Show wiki hii,
rapa huyo nguli ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter alikosoa vikali
matamshi yanayodaiwa kuwa ya Trump akiizita nchi za afrika kuwa ni nchi
chafu (nchi za shimo la choo).
“Ndiyo,
inaumiza sana na inatuangusha. Kila mtu alisikia hasira. Baada ya
hasira inaumiza kweli kama mtu anawadharau watu wote,” alisema na
kuongeza kuwa ingawa amekanusha matamshi hayo, hivyo ndivyo watu
humzungumzia.
Rapa huyo alienda mbali akimkosoa Trump kwa vitendo vya kibaguzi na kumuita kuwa ni mdudu aliyeshindikana kwa dawa (superbug).
Alipinga kauli kuwa Marekani sasa imeongeza idadi ya ajira hasa kwa nchi za Afrika kama inavyodaiwa na Serikali ya Trump.
Leo,
Trump ametumia mtandao wa Twitter kama ilivyo kawaida yake na kumjibu
Jay-Z akimtaja jina, akisisitiza kuwa tangu aingie madarakani idadi ya
Wamarekani Weusi wasio na ajira imeshuka.
“Mtu
mmoja amtaarifu Jay –Z tafadhali kwamba kwa sababu ya sera zangu, idadi
ya watu weusi wasio na ajira wameripotiwa kuwa katika KIWANGO CHA CHINI
KUWAHI KUTOKEA,” inasomeka tweet ya Trump.
0 comments:
Chapisha Maoni