Timu
ya Simba imezidi kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya
kupata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Majimaji kutoka Songea mkoani
Ruvuma Mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa na kuhitimisha Mzunguko
wa Kwanza.
Simba
walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa John Bocco dakika ya 17
akimalizia mpira uliorudi baada ya kugonga mwamba kufuatia beki Mghana,
Asante Kwasi kupiga tik tak kuunganisha kona ya winga Shiza Ramadhani
Kichuya.
Bocco
aliye katika msimu wake wa kwanza Msimbazi tangu asajiliwe kutoka Azam
FC , aliwainua vitini wapenzi wa Simba kwa kufunga bao la pili dakika ya
26 kwa kichwa akimalizia ‘majaro’ ya kiungo Said Hamisi Ndemla.
Hadi
timu zinakwenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa magoli hayo mawili
dhidi ya Majimaji kipindi cha pili kilianza kwa mabenchi yote ya ufundi
kufanya mabadiliko hata hivyo yaliwanufaisha wenyeji zaidi.
Mnamo
dakika ya 52 na 68 Simba walipata magoli hayo mawili kupitia kwa
Mshambuliaji hatari Raia wa Uganda Emanuel Okwi na kuendelea kukalia
usukani wa wafungaji akiwa na jumla ya magoli 12.
Kwa
Matokeo hayo Simba wamefikisha Jumla ya pointi 35 huku wakifuatiwa na
Azama 30 na mahasimu wao wakubwa wa jadi Yanga wakiwa kwenye nafasi ya
tatu kwa pointi 28 na Mchezo mwingine ulipigwa katika dimba la Namfua
ambapo wenyeji Singida United wamefanikiwa kupata pointi tatu baada ya
kuwafunga Tanzania Prinsons goli 1-0.
0 comments:
Chapisha Maoni