Rais
Jakaya Kikwete amesema amefanikiwa kuweka mazingira bora ya ufanyaji wa
biashara hapa nchini hatua ambayo imefanya uchumi wa Tanzania kukua
katika kasi inayotakiwa na hivyo kusaidia uboreshaji wa maisha ya
watanzania.
Rais Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa baraza
la taifa la biashara na kusema kuwa uboreshaji huo umefanyika katika
nyanja mbalimbali ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa miundombinu na uwekaji
wa mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara.
Naye katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue amesema katika
mkutano huo wanatumai watajadili kwa kina kuhusiana na hali ya ufanyaji
wa biashara nchini ilivyo sambamba na kubuni mikakati mingine ya
kuiboresha kama unavyofanya sasa mpango wa matokeo makubwa sasa-brn.
Mbali ya kujadili mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini pia
wajumbe wa baraza hilo la taifa la biashara wanatarajiwa kutumia mkutano
huo kumuaga rais jakaya kikwete ambaye anamaliza muda wake wa
kuliongoza baraza hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni