Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana
tarehe 28 Januari, 2018 ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa
heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani
Tanzania Mhe. Robert Kisanga (pichani) nyumbani kwa marehemu Oysterbay
Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa
pole kwa mke wa Marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja
na familia ya marehemu.
Jaji
Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika
hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia
saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili
wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga
nyumbani kwa marehemu Oysterbay Jijini Dar es Salaam jana Jumapili
Januari 28, 208.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini
kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa
marehemu Oysterbay Jijini Dar es Salaam jana Jumapili Januari 28,
2018.
0 comments:
Chapisha Maoni