Mtoto
mwenye umri wa miaka kumi na moja amekutwa akiwa amejinyonga katika
eneo la Ongata Rongai Kenya katika mazingira ya kutatanisha.
Mtoto
huyo wa kiume ambaye alikuwa akiishi na mama yake pamoja na mdogo wake
wa kike alikutwa juzi jioni akiwa ananing’inia kwenye kamba.
Tukio
hilo lilibainika baada ya mdogo wake huyo mwenye umri wa miaka sita
kurejea nyumbani na kukuta mlango ukiwa umefungwa kwa ndani na jitihada
zake za kujaribu kufungua na kuita hazikufanikiwa kwani hapakuwa na mtu
aliyeitikia.
Kutokana
na kugonga mlango na kuita kwa muda mrefu, majirani akiwamo mwenye
nyumba walikwenda kumsaidia na walikubaliana kwamba waondoe chuma
kilichokuwa katika mlango ili kumwezesha binti kuingia ndani na kumkuta
kaka yake akiwa ananing’inia kwenye kamba.
Majirani
hao walitoa taarifa katika kituo cha Polisi Rongai ambao walifika na
kuchukua mwili wa marehemu na kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia
maiti cha jiji huku wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni