Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu
pamoja na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu
wanaendelea kuwa salama na mali zao. Hata hivyo kwa siku ya jana
kumekuwa na ajali 01 ya barabarani kama ifuatavyo:-
Mnamo
tarehe 18.01.2018 majira ya saa 16:45 jioni huko eneo la Iwambi, Kata
ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu
ya Mbeya kwenda Tunduma, Gari yenye namba za usajili PT 2079 Toyota Land
Rover mali ya Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU – Mbeya ikiendeshwa na
askari namba G. 3452 PC ADAM [30] Mkazi wa Iganzo ikitokea Mbeya Mjini
kuelekea Mbalizi iliacha njia na kupinduka kisha kusababisha vifo kwa
askari wawili ambao ni 1. H. 4335 PC MATHEW JAILOS MPOGOLE [26] na 2. H.
1215 PC PROSPER JORDAN CHALAMILA [29].
Aidha
katika ajali hiyo, askari 09 walijeruhiwa ambapo kati yao majeruhi
wawili wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na majeruhi saba wametibiwa na
kuruhusiwa. Waliolazwa ni 1. H. 6952 PC KELVIN MARTIN [28] Mkazi wa
forest ameumia kichwani na 2. G. 3452 PC ADAM [30] Mkazi wa Iganzo,
Dereva.
Aidha
majeruhi wengine waliotibiwa na kuruhusiwa ni 1. H. 3929 PC LEONARD
MICHAEL [26] ambaye ameumia mkono wa kushoto, 2. H. 469 PC FREDY MBANDE
[28] ambaye ameumia mgongoni, 3. H. 948 PC DAVID IBRAHIM [27] ambaye
amepata maumivu mwilini, 4. G. 9588 PC MARWA [29] ambaye amepata maumivu
mwilini, 5. H. 1325 PC CHRISTOPHER DANIEL MSANGI [26] ambaye ameumia
mbavu, 6. H. 6789 PC LUCAS ANDREA MASHALA, [24] ambaye ameumia kichwani
na mbavu upande wa kulia na 7. G. 6849 PC HAMIS ALLY [32] ambaye
amevunjika mkono wa kulia.
Chanzo
cha ajali ni mwendokasi akijaribu kuyapita magari mengine pamoja na
utelezi katika barabara. Upelelezi unaendelea. Miili ya marehemu
imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na majeruhi wamelazwa Hospitalini
hapo. Taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kwenda nyumbani kwao
Iringa zinafanyika.
WITO:
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA
anatoa wito kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha madereva
kuzingatia udereva wa kujihami hasa kutokana na utelezi na kujiepusha na
uendeshaji wa mwendo kasi. Aidha Kamanda MPINGA anatoa rai kwa
madereva kuzingatia sheria na kanuni zote za usalama barabarani.
Imesainiwa na:
[MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
0 comments:
Chapisha Maoni