WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao.
Ametoa kauli hiyo Jumanne, Oktoba 31, 2017 wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada.
Waziri
Mkuu ambaye yuko Canada kwa ziara ya kikazi, alisema kila Mtanzania
anapaswa ahubiri utaifa wake. “Wakati wote ringia nchi yako, unapotakiwa
kuisemea nchi yako, isemee vizuri kama ambavyo wengine wanasemea vizuri
nchi zao licha ya matatizo waliyonayo.”
Alisema
Serikali inawasisitiza wananchi wake hasa waishio nje ya nchi, wawe
wazalendo na washirikiane kuhakikisha wanazitumia fursa za kimaendeleo
vizuri kwa ajili ya manufaa ya nchi yao.
Awali,
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Nzoka, alitumia fursa hiyo
kuwasihi Watanzania hao wazingatie sheria za nchi wanayoishi.
“Wote
sisi tunawatambua kama mabalozi katika nafasi zenu hapa Canada.
Tunawashauri muwe raia wema, na muishi kwa kufuata sheria na taratibu za
nchi hii na msisahau mlipotoka, kwani hakuna mahali pazuri kama
nyumbani,” alisisitiza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO,
NOVEMBA MOSI, 2017.
0 comments:
Chapisha Maoni