Jina langu ninaitwa Vumy.
Nilikuwa
dada wa kazi ( Hausigeli ) nikamtamani kimapenzi baba mwenye nyumba
kwa sababu alikuwa na pesa na mali nyingi sana. Nilijua nikiwa
nae kimapenzi basi shida zangu zote zitaisha.
Nikaenda
kuomba ushauri kwa rafiki mmoja ambae akanielekeza kwa mganga
mmoja wa kienyeji ili anipe dawa niweze kumkamata kichawi baba
mwenye nyumba.
Rafiki
yangu aliniambia mganga huyo ni hatari sana kwenye dawa za
mapenzi na kwamba endapo nitafanikiwa kuonana nae basi huyo
mwanaume nitamkamata na atafanya kila kitu ninacho kitaka.
Nilipo enda kwa mganga nikapewa dawa ya kumuwekea baba mwenye nyumba kwenye chakula anachokula .
Mganga
akanipa sharti moja akaniambia, nihakikishe hicho chakula hali
mtu mwingine yoyote yule isipokuwa baba mwenye nyumba na
ikitokea nikivunja sharti hilo nitapata madhara makubwa sana
ambayo hakutaka kuyaweka wazi.
Hilo
lilikuwa sharti rahisi sana Kwangu, kwa sababu mara nyingi
baba mwenye nyumba huwa anarudi usiku na huwa anakula chakula
chake peke yake na mara nyingi huwa anamkuta mke wake
ameshakula na amelala.
Siku hiyo usiku mama mwenye nyumba akasema hali chakula kigumu, atakunywa maziwa fresh tu ya moto.
Nikamtayarishia
kama alivyo agiza wakati huo huo baba mwenye nyumba
nikamuandalia ugali na nyama na maziwa mtindi na kuweka dawa
niliyopewa na mganga kwenye nyama ili baba mwenye nyumba akila
hiyo dawa anase na anipende.
Sijui
kitu gani kilimvutia? Sijui ni harufu ya chaklula au alipatwa
na njaa ghafla, mama mwenye nyumba akaniambia amekipenda hicho
chakula,anaomba nimpe ale halafu baba mwenye nyumba nimuandalie
chakula kingine.
Nilichanganyikiwa
lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kumpa chakula nilicho kiandaa
kwa baba mwenye nyumba ambacho nilikuwa nimekiwekea limbwata
ili baba mwenye nyumba anase.
Baada ya kumpa mama mwenye nyumba chakula nikaenda chooni na kumpigia simu mganga kumwambia kilicho tokea.
Nilivyo
mpigia simu mganga akaniambia kwa ukali kwamba alinionya tangu
mwanzo niwe makini na hiyo dawa na kuniambia nisubiri
kitakacho nitokea.
Kesho
yake asubuhi yule mama mwenye nyumba akaanza kuonyesha upendo
na mapenzi ya hali ya juu sana Kwangu kiasi nikaogopa. Mapenzi
ya mama mwenye nyumba Kwangju yalikuwa yanaongezeka saa hadi
saa kiasi akawa anafanya vitu ambavyo mimi ndo natakiwa
kuvifanya kama vile kuosha vyombo, kufua nguo, kupika nakadhalika.
Baada
ya kama siku tatu hivi , uzalendo ukamshinda akaamua kunitamkia
laivu kwamba ananipenda sana na kwamba anataka tuanzishe
uhusiano wa kimapenzi.
Nilimwambia
siwezi kufanya hivyo, sijawahi kufanya hivyo wala sitarajii
kuwa katika mahusiano na mwanamke mwenzangu lakini wala
hakuweza kunielewa.
Akaniahidi
vitu vingi sana.Kunisomesha chuo, kumlea na kumsomesha mtoto
wangu,kunijengea nyumba, kuninunulia gari, mashamba, viwanja,
kunifungulia akaunti benki na biashara.
Vyote nikakataa na kumwambia siwezi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwenzangu.
Nilivyo
ona usumbufu umezidi nikaamua kuondoka na kurudi nyumbani kwetu
kijijini Kondoa, lakini kwa kuwa alikuwa anajua natoka sehemu
gani Kondoa, na namba za simu za mama angu alikuwa nazo,
akanifuata hadi Kondoa na kuniomba nirudi kufanya kazi kwake.
Akanipa
hela nyingi na mama angu pia akampa hela. Mimi nikamwambia
kuna mambo nayamalizia kijijini Kondoa yeye arudi zake dar
nitamfuata baada ya wiki moja, akakubali kwa shingo upande.
Alivyo
ondoka kijijini nikamwambia mama angu siwezi kwenda kwa huyo
mwanamke kwa sababu nimeambiwa ni freemason. Sikutaka mama angu
ajue kitu gani kinaendelea.
Ilivyo pita wiki moja sijaenda akaanza kusumbua kwa simu, nikawa sipokei.
Akaanza kumsumbua mama angu na kumuomba anibembeleze nirudi kufanya kazi kwake.
Katika
kumlainisha mama angu akawa anamtumia hela nyingi tu mpaka
mama angu akahamia upande wa huyo mwanamke na kunishawishi
niende kufanya nae kazi.
Kama
hiyo haitoshi amemjengea nyumba mama angu kijijini na huwa
anakuja kijijini kwetu linapotokea tatizo lolote la kifamilia
au sherehe.
Yote hayo anayajua kwa sababu anawasiliana sana na mama angu.
Hiyo
ilikuwa mwaka 2015 mwishoni lakini mpaka sasa hivi bado
ananisumbua na nimeshamwambia kuwa sipo tayari kufanya upuuzi
huo.
Yupo kama aliye changanyikiwa au aliye pagawa na pepo.
Amegombana na kutengana na mume wake kwa sababu yangu .
Kuna kipindi alikuwa ananipigia simu kunibembeleza niwe nae mbele ya mume wake.
Mume wake alipofariki ndugu walimzuia kushiriki kwenye mazishi kwa kumtuhumu kusababisha kifo cha mume wake.
Lakini bado ananin’gan’ania tu licha ya kumwambia mimi sipo tayari kufanya anavyo taka yeye.
Kuna
kipindi nilirudi kijijini kulima ufuta na kukaa huko kwa
miezi mitatu na yeye akaja kukaa kijijini na kuchukua mashamba
alime ufuta lakini lengo lilikuwa kuwa karibu na mimi.
Katika kipindi chote hicho usumbufu ambao amekuwa akinipa ni mkubwa mno.
Amekuwa kama zezeta au mtu aliye pagawa hivi.
Nimejaribu kila njia ya kumkwepa huyu mama lakini imeshindikana. .
Nimemwambia si awatafute wanawake wenye tabia hizo anasema ananitaka mimi na sio mtu mwingine yoyote yule.
Nimejaribu
kwenda kwa mganga alio nipa hiyo dawa na kumwambia
anitenganishe na huyu mwanamke amekataa kata kata anasema huo
sio utaratibu wake wa kazi na kwamba uchawi huo ni wa maisha
na hauwezi kubatilishwa kwa namna yoyote ile hadi naingia
kaburini.
Utaisha
nguvu pindi mmoja wetu atakapo itwa na Mungu kwa hiyo
nivumilie tu kwa sababu mimi ndio nilifanya uzembe.
Siwezi kuendelea kuishi katika hali ya usumbufu mkubwa kiasi hiki.
Tena
mganga kaniambia halafu nina bahati kwa sababu kuna wengine
huwa wanafanyaga uzembe dawa anakula baba mzazi au mtoto au
kwa wanaume dawa anakula mama mzazi , mtoto au dada ambao
wengi wao huishia kukimbia nchi au hata kujaribu kujiua.
Kwa hivyo nishukuru walau nina bahati.
Nimejaribu kwenda kwa waganga na waganga lakini wapi.
Imeshindikana kumzuia mwanamke huyu asiendelee kunin’gan’gania.
Nimejaribu kuombewa kote imeshindikana.
SASA
NDUGU ZANGU. NINAOMBA MSAADA WENU. NITUMIE NJIA GANI ILI
KUMFUNGA HUYU MAMA ASIENDELEE KUNIFUATA FUATA NA KUNIGANDA ?
AU
KUNA NJIA YOYOTE INAYO WEZA KUTUMIKA KUMZINDUA HUYU MWANAMKE NA
KUMFANYA ARUDI KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA ? YAANI AJITAMBUE
KWA SABABU NAONA ANAE ANYA HIVYO SIO YEYE ILA NI HUO UCHAWI
NILIO MLISHA KWA BAHATI MBAYA ..
JAMANI
KAMA KUNA MTUMISHI YOYOTE WA MUNGU ANADHANI ANAWEZA WALAU
KUMUOMBEA HUYO MAMA ILI ARUDI KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA,
MIMI NIPO TAYARI KUMUELEKEZA MAHALI ANAPOISHI HUYO MAMA AWEZE
KUFANYA UTARATIBU WA KWENDA KUMUOMBEA NA KUMRUDISHA KATIKA HALI
YAKE YA KAWAIDA
NA
KAMA KUNA MTU ANAWEZA KUFANYA MAOMBI YA KUMZUIA HUYO MAMA
ASIENDELEE KUNIFUATILIA TAFADHALI SANA NAOMBA AWASILIANE NAMI.
HATA KAMA UNAJUA MAHALI NINAPO WEZA KUPATA MSAADA TAFADHALI NIFAHAMISHE.
Niandikie kupitia barua pepe yangu :
0 comments:
Chapisha Maoni