Tanzania
imeiomba Mahakama ya Jimbo la Columbia kutupilia mbali ombi la Stirling
Civil Engineering la kutaka kusajili hukumu mbili za Mahakama ya
Kimataifa Usuluhishi ili kampuni hiyo ya Uingereza ikamate mali nyingine
za Serikali zilizopo nchini Marekani.
Stirling,
ambayo ni kampuni ya ujenzi iliyokatishwa zabuni ya kujenga Barabara ya
Bagamoyo kutoka eneo la Wazo Hill kutokana na kutekeleza mradi huo
chini ya kiwango, ilishinda ksi iliyofungua kupinga kitendo hicho
msuluhishi akaagiza ilipwe dola 38 milioni za Kimarekani.
Kampuni
hiyo ilisajili uamuzi huo wa msuluhishi nchini Uingereza na Uholanzi na
kufanikiwa kushikilia ndege aina ya Bombardier Q400 iliyonunuliwa na
Serikali na sasa inataka mahakama isajili hukumu mbili za mwaka 2015 na
2016 zisajiliwe Marekani ili ipate nguvu ya kushikilia mali nyingine.
Lakini Serikali ya Tanzania imeamua kupambana na kampuni hiyo mahakamani kuizuia isiendelee kukamata mali zake.
Kwa
mujibu wa tovuti ya Law360, ambayo ni maalum kwa ajili ya habari za
kisheria, Tanzania imewasilisha pingamizi, ikitaka mahakama hiyo
isisajili hukumu hiyo ya Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi.
Katika hoja yake, Tanzania imesema mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kushughulikia ombi hilo la Stirling.
Serikali
inasema ina kinga dhidi ya hukumu mbili zilizotolewa na mahakamani
nchini Uingereza na Uholanzi ambazo kampuni hiyo inaomba zitambuliwe pia
Marekani, ikisema kuwa ondoleo hilo la kinga linalotolewa na Sheria ya
Kinga ya Mataifa ya Kigeni, haiwezi kutumika.
Kwa
mujibu wa tovuti hiyo, Sheria ya Kinga ya Mataifa ya Kigeni inasema
taifa la kigeni halitakuwa na kinga dhidi ya mamlaka ya mahakama ya
Marekani katika mashauri yanayowasilishwa kwa ajili ya kuthibitisha tuzo
za mahakama ya usuluhishi zinazoongozwa na makubaliano yaliyoidhinishwa
na nchi yanayotambuliwa nchini Marekani.
Serikaloi
inasema Stirling inataka kutambuliwa kwa hukumu za mahakama ya nje ili
ziwe na nguvu, badala ya kuomba kutekelezwa kwa hukumu hizo.
“Kuna
tofauti inayotambulika vizuri kati ya kuthibitisha tuzo ya msuluhishi,
kwa upande mmoja, na kutambua hukumu ya mahakama ya nje, kwa upande
mwingine,” tovuti hiyo inakariri hoja hizo za Serikali.
“ingawa tuzo ya msuluhishi na hukumu ya mahakama zinalingana kwa kiasi kikubwa, hata hivyo zina tofautiana.”
Kwa hiyo, Serikali inasema Stirling haiwezi kutumia mwanya huo, kuomba utekelezaji wa hukumu hizo.
Kampuni
hiyo inadai kuwa kitendo cha Serikali ya Tanzania kukubali kwenda
kwenye Mahakama ya Usuluhishi, kiliondoa kinga hiyo na kuipa yenyewe
haki ya kulipwa fidia hiyo.
Mwaka
1999 Serikali iliipa kandarasi kampuni ya Impresa Ing. Fortunato
Federici SpA (IFF) ambayo baadaye ilinunuliwa na Stirling, kukarabati
barabara ya Wazo Hill-Bagamoyo, lakini baadaye ikatimuliwa.
Mwaka
2004 kampuni hiyo ilifungua kesi Mahakama ya Usuluhishi wa Kimataifa na
hukumu ilitolewa mwaka 2009 na 2010, lakini Serikali haikulipa fidia
iliyopendekezwa na kuilazimu kukazia hukumu Uingereza na Uholanzi.
Novemba 2015, mahakama nchini Uingereza iliridhia utekelezaji wa hukumu hiyo na Uholanzi ilifanya hivyo Desemba 2016.
0 comments:
Chapisha Maoni