Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa
Upako’ bado anaamini kuwa Mtanzania kufa masikini ni ujinga na ufala,
hii ni kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya nchi.
Mzee
wa Upako amesema Tanzania tuna mbuga za wanyama, madini ya Tanzanite,
ardhi yenye rutuba hivyo haiwezekani mtu kufa masikini.
“Kufa
masikini sio ujinga tuu ni ufala, sasa ufe masikini si fala tuu, halafu
ukute ulipata nafasi na fursa mbalimbali huko,“amesema Mzee wa Upako
kwenye kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM na kusisitiza.
“Tuna
mbuga za wanyama , tuna Tanzanite, tuna almasi, tuna ardhi bora,
Tanzania ni nchi ya pili katika Afrika kuwa na mifugo mingi, halafu bado
sisi ni masikini? mimi akili haikubali.“amesema Mzee wa Upako na kutoa
mfano.
“Kuna
nchi moja Singapore wanaendesha nchi yako kwa bandari tu lakini
matajiri wanaikimbilia Japan, kwa hiyo mimi siamini Katika umasikini,
sisi sio wazima tumerogwa.” amemaliza Mzee wa Upako.
0 comments:
Chapisha Maoni