Kada
Maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani
Dodoma amewasihi Watanzania kumpuuza Mwanasiasa Lazaro Nyalandu ambaye
juzi ametangaza kujivua nyadhifa zake zote katika CCM ikiwemo ujumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa
kile alichodai Serikali kukigandamiza Chama na CCM kupoteza mwelekeo.
Lusinde
amesema Bw. Lazaro Nyalandu hakuwahi kunyimwa nafasi yoyote ya kutoa
maoni yake ama dukuduku zake ndani ya chama wala bungeni na kwamba
uamuzi huo unaashiria kuwa anatafuta kinga ya kutochukuliwa hatua
kutokana na tuhuma nzito zinazomkabili.
Kada
huyo wa CCM amesema ana wasiwasi ndani ya Serikali wapo watendaji ama
viongozi wasio waaminifu ambao watakuwa wamevujisha taarifa za hatua
ambazo Serikali inatarajia kuzichukua dhidi kutokana na makosa makubwa
aliyoyasababisha alipokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na alipokuwa
Naibu Waziri.
==>Msikilize Lusinde hapa chini akizungumza;
0 comments:
Chapisha Maoni