Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Eleuther
Mwageni amesema wanafunzi ambao tayari wamekidhi vigezo na kupitishwa
kujiunga na elimu ya juu wanatakiwa kuripoti chuoni ili kuanza masomo
ifikapo Oktoba 30.
Prof.
Mwageni ameyasema hayo leo wakati anatoa ufafanuzi juu ya tarehe ya
kufunguliwa kwa vyuo kutokana na mkanganyiko ambao wameupata baadhi ya
wanafunzi kuhusu muda sahihi wa masomo kuanza kwa mwaka wa masomo
2017/18 hususani wale ambao wameomba nafasi kwenye awamu za pili na tatu
za Udahili.
“Tarehe
ya Kalenda ya masomo haijabadilika iko palepale ambayo ni Oktoba 30
wanafunzi wanatakiwa kuanza masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018”,
amesema Mwageni.
Aidha
Prof. Mwageni ameeleza kuwa zaidi ya wanafunzi 450,000 tayari
wameshapata vyuo hivyo kinachosubiriwa katika awamu ya tatu ni kupitisha
wanafunzi wengine 12,000 ili kufikia malengo ambayo ni wanafunzi
57,000.
Awamu
ya tatu ambayo ilianza Oktoba 18 hadi 22 imefikia hatua nzuri ambapo
vyuo vinawasilisha TCU majina ya waombaji ambao vimewapitisha ili tume
iweze kujiridhisha kisha wanafunzi waliochaguliwa katika awamu hiyo
wajiunge na vyuo na waanze masomo kwa wakati.
Mapema
mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
alishauri TCU iweke utaratibu wa wanafunzi kuomba nafasi chuoni moja kwa
moja ili waende vyuo wanavyotaka wao tofauti na awali ambapo zoezi la
kupanga vyuo lilikuwa linasimamiwa na Tume hiyo ya Vyuo Vikuu TCU
0 comments:
Chapisha Maoni