Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imelaani kitendo cha jeshi la
polisi kumkamata na kumhoji mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe,
Agusta Njoji kutokana na habari aliyoiandika mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo Nagenjwa Kaboyoka aliwaambia waandishi wa habari jana
kuwa kitendo kilichofanywa na polisi Mkoa wa Dodoma ni kutaka kuminya na
kuficha maovu ambayo yamejaa ndani ya jeshi hilo.
Njoji
aliandika habari kutoka kwenye kamati hiyo wakati PAC ilipokutana na
viongozi wa polisi kwa lengo la kutaka ufafanuzi kuhusu manunuzi ya
magari ya polisi maarufu washawasha pamoja na mchakato wake wakihoji
kutokana na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali(CAG).
Kufuatia
taarifa hiyo, Polisi Mkoa wa Dodoma walimuita na kumhoji na kisha
kuamuru awekwe ndani kabla ya Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi Dodoma
(CPC), Habel Chidawali kumwekea dhamana kwa bondi ya Sh 5 milioni.
Nagenjwa
alikiri kuwa taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Nipashe na Mwananchi
mwishoni mwa wiki zilikuwa sahihi lakini akashangazwa kwa polisi kuamua
kuwasumbua waandishi wa habari.
“Nisema
kuwa, kazi zetu kwa sehemu kubwa zinawategemea waandishi wa habari,
tumesikitishwa sana na tumeamua kumwandikia barua Spika wa Bunge kutaka
ufafanuzi ili kuondoa mkanganyiko wa utendaji wa kazi zetu kuliko
kuingiliwa mara kwa mara na wengine,” alisema Kagoyoka
Kwa
mujibu wa maelezo ya Kaboyoka, kabla ya kumuandikia spika barua ya
kutaka maelezo ya utendaji kazi wa kamati, walimtuma ofisa wa bunge
kwenda kuzungumza na polisi ili kujua ukweli wa mambo ulivyo na kwamba
polisi walikiri kukosea na wakaahidi kulifuta jalada hilo.
Wakati
kamati ikiwaita waandishi kuzungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa CPC,
Habel Chidawali na katibu wake Bilson Vedastus waliitwa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Mroto kwa ajili ya kuzungumzia sakata
hilo.
Kwa
mujibu wa Chidawali, Mroto aliwataka waandishi kuendelea na majukumu
yao kwani wito kwake kwa mwandishi huyo ulilenga kujua ukweli wa chanzo
cha habari hiyo na hivyo akasema kuwa yamekwisha.
0 comments:
Chapisha Maoni