Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi ikidaiwa ni kutokana na agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella.
Hata
hivyo, Mongella amekana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo
anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza.
Mariam
Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa
na meya Bwire amesema kuwekwa kwake ndani kunatokana na agizo la mkuu wa
mkoa.
“Nimepata
taarifa za meya kuwekwa mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua
kinachoendelea,” amesema Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017.
Taarifa
zinasema meya Bwire amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa
mapokezi ya Rais John Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo.
Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.”
Tangu
Aprili, Bwire na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba wamekuwa
katika mgogoro kila upande ukiutuhumu mwingine kuhujumu shughuli za
maendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni