Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
18 Novemba, 2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai (DCI) Bw. Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kagera.Uteuzi wa Bw. Diwani Athuman unaanza mara moja.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi tano za Serikali kama ifuatavyo.
Kwanza, Rais
Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo (SUA)
Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.
Pili,
Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Bw. Sylvester M.
Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA).
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016
Tatu,
Rais Magufuli amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO).
Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.
Nne, Rais Magufuli amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
Tano,
Rais Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti
wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya
Kitropiki Tanzania (TPRI)
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Novemba, 2016