Aliyekuwa
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
Shy-Rose Bhanji amelalamika jina lake kukatwa katika kinyang'anyiro cha
kutetea nafasi hiyo katika muhula ujao bila kuhojiwa juu ya tuhuma
zilizopeleka jina lake kukatwa.
Licha
ya malalamiko hayo, pia Shy-Rose Bhanji ametumia fursa hiyo kuwapongeza
watu waliochaguliwa kuwa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuwashukuru wabunge kwa kumpigia kura
zilizomuwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo waliopata
kura nyingi zaidi.
"Ingawa
jina langu limekatwa na Kamati Kuu ya Chama bila ya mimi nwenyewe
kuitwa na kuhojiwa ili nipewe haki ya kujibu hoja zozote dhidi yangu,
nawapongeza wote waliochaguliwa kuwa wagombea wa EALA kupitia CCM.
Ninawashukuru sana Wabunge kwa kunipigia kura nyingi zilizoniwezesha
kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo walioongoza kwa kura" aliandika Shy-Rose Bhanji