SIKU
chache tu baada ya Rais John Pombe Magufuli kufanikisha kukamilika kwa
ufanisi sehemu ya kwanza majadiliano na kampuni ya Barrick Gold kuhusu
biashara ya madini hayo nchini, majarida na magazeti mbalimbali maarufu
duniani yamemzungia kwa staili tofauti.
Katika
makubaliano hayo, huku Mwenyekiti wa Barrick Gold, Prof. John Thornton,
akilazimika kusafiri kwa ndege binafsi kuja mara 2 nchini Tanzania,
Tanzania imefikia kile ambacho nchi chache sana duniani zimeweza
kufanikisha katika kunufaika na sekta ya madini.
Pamoja
na kupewa hisa zinazofikia asilimia 16 katika migodi yote ya Barrick
nchini, makubaliano hayo pia yanaruhusu Tanzania kuchukua madini yote
yanayopatikana baada ya makinikia kuuzwa na itapata faida ya nusu kwa
nusu na Barrick baada ya dhahabu ya kawaida kuuzwa.
Aidha,
kampuni ya Barrick itaweka ofisi zake mpya katika jiji la Mwanza
Tanzania na kwamba idadi ya watanzania wanaoshiriki katika Bodi na
menejimenti ya Shirika hilo itaongezeka ili kulinda maslahi ya pande
zote mbili.
Ndio
maana katika makala yake iliyoitwa “Tanzania’s squeeze on mining firms
seems to be working as it gets $300 million in back taxes” Jarida
mashuhuri la masuala ya madini Quartz lilimueleza Rais Magufuli kama
kiongozi aliyefanikiwa kuyabana makampuni makubwa kwa maslahi ya
wananchi wake na hayumbishwi.
“Rais
wa Tanzania mwenye msimamo usioyumba katika madini, Dkt. John Pombe
Magufuli anaongoza vita inayohakikisha kuwa makampuni makubwa yanapata
haki yao lakini wananchi wa Tanzania nao wanapata faida katika sekta ya
madini,” anaandika Abdi Latif Dadir mwandishi wa jarida hilo lenye makao yake makuu Marekani.
Kwa
upande wake mtandao wa habari za uchumi na biashara wa Bloomberg
ulisema kuwa Rais Magufuli ni kiongozi ambaye “anaifanyia mageuzi
makubwa sekta ya madini ili kuwafaidisha wananchi.”
Mtandao
huo pia umeongeza kuwa licha ya azma hiyo, Serikali ya Magufuli pia ina
mikakati mipana zaidi katika “kutekeleza sera ya viwanda na miradi ya
kiuchumi katika nchi ya Tanzania ambayo ni ya sita kuwa na uchumi mkubwa
katika Ukanda wa Afrika Kusini mwa Sahara.”
Gazeti
mashuhuri la New York Times lilianza kwa kusema Serikali nyingi katika
nchi za Afrika na Asia-kutoka Afrika Kusini hadi Indonesia zimeanzisha
harakati za kuhakikisha zinafaidika zaidi na madai yao.
Gazeti
hilo limeeleza hatua mbalimbali alizozichua Rais Magufuli ikiwemo
kuzuia usafirishaji wa mchango wa madini maarufu kama makinikia. “Rais
wa Tanzania hata hivyo hakusema iwapo uuzaji nje wa madini hayo
utaruhusiwa tena ama la,” limeripoti New York Times.
0 comments:
Chapisha Maoni