Askari
katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam, Sajenti
Nyagea amefika Mahakamani Kuu na kusoma maelezo ya Josephine Mushumbusi
katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa fani ya
uigizaji filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu.
Mushumbusi
katika maelezo hayo alisema Steven Kanumba alikuwa akifanya mazoezi ya
kutanua misuli na alimshauri kuyaacha. Pia, alimweleza kuwa anasumbuliwa
na maumivu ya moyo.
Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa filamu, Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Mbele ya Jaji Sam Rumanyika, Sajenti Nyagea leo Jumatano Oktoba 25,2017 amesoma maelezo ya Mushumbusi aliyoyatoa polisi.
Wakili
Peter Kibatala anayemwakilisha Lulu katika kesi hiyo aliieleza Mahakama
kuwa Mushumbusi hapatikani kwa kuwa yuko nchini Canada, hivyo aliomba
maelezo yake yapokewe kama sehemu ya ushahidi.
Katika
maelezo hayo yaliyorekodiwa na Sajenti Nyagea, Mushumbusi alieleza
alikuwa na kituo cha tiba mbadala na alikuwa akimtibu Kanumba.
Ameeleza
Kanumba alikuwa akisumbuliwa na matatizo mbalimbali na wakati
akimhudumia alibaini alikuwa akifanya mazoezi ya kutanua misuli na
alimshauri kuyaacha.
Mushumbusi katika maelezo hayo anasema Kanumba alimweleza alihisi kuwa na maumivu ya moyo na alimuomba ampe ushauri.
Katika
maelezo hayo, amesema siku Kanumba alipokwenda kwake alikuwa na watu
wengi, hivyo alimuomba apange siku nyingine na kabla ya kuonana alisikia
kuwa amefariki dunia.
Upande wa utetezi umefunga ushahidi wake na kesho Oktoba 26,2017 wazee wa baraza watatoa maoni yao.
0 comments:
Chapisha Maoni