Katika
siku za hivi karibuni kumejitokeza kikundi cha watu wanaotumia vibaya
jina la Jeshi la Polisi kwa kujifanya ni Maafisa wa Jeshi la Polisi na
kuwatapeli watu kwa kigezo cha kuwapatia ajira.
Watu
hao wamesambaza taarifa kupitia mitandao ya kijamii inayosomeka ‘Vigezo
sifa za kujiunga na Jeshi la Polisi’, huku ndani yake ikitaja sifa
ambazo kwa mujibu wa kikundi hicho ndizo anazopaswa kuwa nazo mtu
anayeomba nafasi ya kujiunga na Jeshi la Polisi.
Jeshi
la polisi linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa taarifa hizo ni za
uongo na zenye lengo la kupotosha Umma kwa madhumuni wanayoyajua wao
wenyewe. Pia zipo taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa wapo watu
wanaoombwa kutoa fedha na matapeli hao ili waweze kuwapatia nafasi ya
ajira hizo.
Wananchi
watambue kuwa Jeshi la Polisi lina utaratibu wake mzuri na wa wazi wa
kuajiri. Pale Serikali itakapotoa idhini ya kuajiri watumishi wapya
utaratibu huo utatangazwa kwa wananchi ili waweze kuufuata kuomba
nafasi hizo.
Jeshi
la Polisi linawataka wananchi kutoa taarifa juu ya kikundi hicho
kupitia kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nawe au ofisi za
Serikali ili watu hao waweze kukamatwa na hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao.
Wananchi
mnashauriwa kupata taarifa sahihi za Jeshi la Polisi kupitia website
yake ambayo ni www.policeforce.go.tz au akaunti ya twitter
www.twitter.com/tanpol pamoja na Facebook www.facebook.com/tanpol
Imetolewa na:
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
Dar es Salaam
0 comments:
Chapisha Maoni