Mgombea
Urais wa Kenya anaeungwa mkono na ngome ya NASA, Raila Odinga amepinga
matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya nchi hiyo
(IEBC).
Akizungumza
na waandishi wa habari saa chache zilizopita, Odinga amesema kuwa Tume
haikufuata utaratibu wa kutangaza matokeo kwani wawakilishi wa vyama
walio kwenye vituo hawakupewa fomu namba 34A ili wasaini matokeo
yaliyotangazwa.
Odinga ameeleza kuwa kutokana na kutokuwepo fomu hizo ni vigumu kubaini matokeo yanayotangazwa na IEBC yanatoka wapi.
“Mfumo
umeachwa na sasa ni mitambo ndio inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba
hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje
matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu namba 34A pekee inazoonesha
chanzo cha matokeo,” amesema Odinga.
“Kwa
hivyo, tunakataa matokeo yote yaliyotangazwa kwa sasa na kuitaka tume
ya IEBC itoe fomu 34A za kila kituo kabla ya matokeo zaidi kutangazwa,” aliongeza.
Hata
hivyo, Msemaji wa Jubilee amesema kuwa madai ya NASA hayana mashiko
kwani hakuna sehemu ambayo walishinda mwaka 2013 ambapo mwaka huu
wameshindwa bali wamefanya vizuri pia kwenye maeneo ambayo walishindwa
vibaya mwaka huo.
Hivyo,
aliwataka NASA kutoendelea kutoa maeneno aliyodai ni ya udanganyifu
bali kujiandaa kukubali matokeo kwani itakayoshinda ni ‘Kenya’ na sio
chama chochote cha uchaguzi.
Alisema
kuwa fomu namba 34A iko katika mfumo wa kielektroniki hivyo yeyote
akatayetaka kuichakachua ataonekana. Jubilee wanaonesha kuwa na uhakika
wa kushinda katika uchaguzi huu ingawa matokeo yanaendelea kutangazwa
huku zaidi ya asilimia 91 ya kura zote ikiwa imeshahesabiwa.
Tume
imeendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi huo kwa njia ya matandao kama
yanavyotoka katika vituo ambapo hadi sasa Kenyatta anaonekana kuongoza
akiwa na asilimia 54.57 huku Odinga akiwa na asilimia 44.58. Wawili hao
wanatofautina zaidi ya kura milioni moja.
0 comments:
Chapisha Maoni