Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu
Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana kwa kesi
inayowakabili, wamerudishwa rumande mpaka Julai 17 mwaka huu shtaka lao
litakaposomwa tena.
Uamuzi
huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es
Salaam, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria dhidi ya
mawakili wa utetezi na mawakili upande wa jamhuri (serikali).
Malinzi
na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya
madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani
kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na
kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.
0 comments:
Chapisha Maoni