Baraza
la Vijana la Chadema(Bavicha), wamesema wanatarajia kufanya maandamano
ya amani yenye lengo la kuipongeza kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Akizungumza
leo Jumatatu katika mahafali ya Umoja wa Wanachama wa Chadema Vyuo
Vikuu (CHASO), Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward
Simbeyi alisema kuwa watafanya maandamano mapema mwa mwezi huu ili
kuipongeza kambi hiyo ambapo amesema imekuwa ikipigania rasilimali za
nchi.
Simbeyi
ambaye ni mratibu wa CHASO taifa,alisema wanakusudia kufanya hivyo kama
chama cha CCM kilivyofanya maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli kwa
kuzuia mchanga wa madini (Makinikia).
Alisema
kuwa wabunge wa upinzani wamekuwa wakipambana kwa kujenga hoja bungeni
kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao wenyewe badala ya
watu wachache kunufaika.
Hata
hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alisema kuwa
maandamano yalishapigwa marufuku na hayaruhusiwi kufanyika mahali
popote.
“Kama walijitokeza watu wakitaka kufanya maandamano ya kumpongeza Rais wakazuiliwa na wao pia wasijaribu kufanya hivyo,”alisema Issah.
0 comments:
Chapisha Maoni