Jeshi
la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, linawashikilia watu
wawili wakazi wa Mtaa wa Nkende mjini Tarime wakidaiwa kumkata mkono
Mkaguzi wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana-River cha nchini Kenya, James
Mnuve (50), wakati wakimgombania mwanamke.
Kamanda
wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo la kukatwa mkono Mkaguzi huyo wa Polisi wa nchini Kenya.
Mwaibambe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Julai 13 mchana katika mtaa wa Nkende mjini Tarime ambapo vijana hao walitenda kosa hilo.
Mwaibambe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Julai 13 mchana katika mtaa wa Nkende mjini Tarime ambapo vijana hao walitenda kosa hilo.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Michael Omahe, anayedaiwa kumtorosha mwanamke
huyo, Anne Njeri, kutoka Kenya na kumleta Tanzania kisha kuishi naye
kinyumba huku akisaidiana na rafiki yake, Daniel Onchiri.
“Mwanamke
huyo (Njeri) anadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi pia na askari
James Mnuve na walikuwa wakiishi huko Tana River nchini Kenya, baada ya
kuondoka, Julai 13 mchana askari huyo alimfuatilia kutoka Kenya hadi
Mtaa wa Nkende, Tarime alipokuwa anaishi na kijana aliyemtorosha
(Michael Omahe),” alisema Kamanda.
Akaongeza,
“Alipofika Mtaa wa Nkende alimkuta Michael, pamoja na rafiki yake huyo
wakiwa na mwanamke huyo na hapo ndipo ugomvi ulipoanza kwani askari
James alitaka kuondoka na mwanamke huyo na zikazuka vurugu kubwa na
kusababisha Mnuve kukatwa kwa kutumia panga.”
Aidha Kamanada huyo alisema kuwa,
“Jeshi la Polisi tulifika kwenye eneo la tukio mapema na kuweza
kuwakamata watuhumiwa wote watatu; Marandi, Ochiri na mwanamke huyo na
kisha tukawahoji kabla ya kuwafikisha mahakamani huku majeruhi akiwa
amepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa matibabu.”
Majeruhi
James anadai kuwa yeye ni Inspekta wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana
River nchini Kenya na mwanamke huyo, Njeri Wanjoi, ni mke wake.
0 comments:
Chapisha Maoni