Chelsea Football Club and Real Madrid have agreed terms for the transfer of Alvaro Morata to Stamford Bridge.
The move is now subject to him agreeing personal terms and passing a medical.
Morata, 24, is a Spanish international forward, and helped Real to lift a second successive Champions League last season.
Hii leo jioni klabu za Real Madrid na Chelsea zimeweka wazi kwamba zimefikia makubaliano kuhusu Alvaro Morata na sasa ni wazi kwamba mshambuliaji huyo yuko njiani kusaini Chelsea masaa machache yajayo.
Morata amekuwa akipata tabu sana kupata namba katika kikosi cha Zinedine Zidane na imemladhimu kuondoka na kwenda kutafuta mahali ambapo atapata namba na Chelsea wako tayari kutoa £80m kumnunua.
Chelsea ilikuwa lazima wapate striker katika dirisha hili la usajili baada ya striker wao tegemezi Diego Costa kuwa mbioni kuondoka baada ya mahusiano yake na kocha wa klabu hiyo kuwa mabaya.
Msimu uliopita Diego Costa alipata dakika 3089 za kuitumikia Chelsea na katika dakika hizo Costa alifunga mabao 20 na kutoa assist 7 na akiwa mchezaji muhimu kabisa akiisaidia Chelsea kubeba ubingwa wa Uingereza.
Anakuja Morata ambaye hakuwa akipewa sana nafasi lakini dakika 1334 alizoitumikia Madrid ambazo ni karibia nusu ya aluzocheza Costa alifunga mabao 15 yakiwa ni mabao 5 tu nyuma ya Costa na kutoa assist 4.
Ukiwaangalia washambuliaji hawa wawili ufumaniaji wao wa nyavu hautofautiani sana japo Morata anaonekana anafunga kwa muda mfupi sana lakini usajili huu unaweza kuwa sahihi sana kwa Chelsea,lakini je ataiweza ligi inayotumia nguvu kama hii ya Epl kama alivyokomaa Costa?
Kuhusu hili la kuihimili ligi ya Uingereza linaweza kuchukua muda kwake kwani tofauti na Costa, Morata ni mchezaji anayetumia akili na spidi sana awapo uwanjani na sio mpambanaji sana kama ilivyo kwa Diego Costa.
Ligi ya Epl ukiangalia top scorers msimy uliopita Kane,Lukaku,Sanchez,Zlatan na Costa wote ni wachezaji aina tofauti na Morata,wachezaji wengi wenye magoli Uingereza wako vizuri sana katika matumizi ya nguvu na ndio sababu kubwa imewafanya kuzoea kufunga.
Unapokuja Uingereza huku una akili na speed ni rahisi sana kuzimwa na mabeki wa ligi hii ambao wanatumia nguvu nyingi, Morata ni bora sana hilo halina mashaka lakini siamini kwamba ubora wake Uingereza utaonekana mapema inaweza kumchukua muda kuzoea.
Na kwa rekodi tu kama haujui ni kwamba washambuliaji watatu ambao wamesajiliwa kwa pesa kubwa Chelsea wote hawakufanya vizuri Fernando Torres,Adriy Shevchenko na Michy Batshuayi hao ndio waliokuwa wanashikilia rekodi ya usajili pesa nyingi Chelsea kabla ya dirisha hili la usajili ila walichofanya klabuni hapo mashabiki wa Chelsea wanakijua.
0 comments:
Chapisha Maoni