Mtunzi: EDDAZARIA G.MSULWA
“Samahani kaka sijui wewe ni nani mwenzangu?”
“Unaniuliza mimi ni nani ndani ya nyumba yangu?”
Moyo
ukanipiga paaaa kama jiwe lililotua juu ya bati tena la nyumba ya
uswahilini.Nikajua jamaa anaweza akawa mume wa Madam Mery mapigo ya moyo
yakazidi kunienda mbio pale jamaa alipoanza kupiga hatua za kwenda
chumbani kwa Madam Mery kwani boxer na tisheti ya shule vyote vipo ndani
ya chumba hicho na vipo sehemu ya wazi kwa mtu yoyote anayeingia lazima
ataviona,na kingine kilichozidi kunipagawisha ni kitanda nilivyo kiacha
kimevurugika kwani kinaonyesha hivi hivi kilikuwa ni kiwanja cha mechi
za wakubwa
ENDELEA
Jamaa kabla hajafunua pazia ili aingie ndani simu yake ikaita.Akaitoa
kwenye mfuko wa suruali kisha akaipokea na kuanza kuzungumza mazungumzo
ambayo yalianza na ndio bosi.Jamaa akanitazama kisha akatoka nje
nikahisi mazungumzo yake ni muhimu sana na ya siri sana ndio maana
akatoka nje huku begi lake akilivua na kuliweka pembeni ya mlango wa
kuingilia chumbani kwa Madam Mery.
Ikawa
nafasi kwangu kuingia chumbani nikachukua kila kilicho changu huku
shuka lililo changungaka nikilitoa na kulisokomeza mvunguni mwa kitanda
na kuliacha godoro likiwa na foronya yake tu pasipo kuwa na
shuka,Nikarudi hadi sebleni na kumuona jamaa akirudi ndani kwani mlango
aliuacha wazi kidogo.Ikanibidi boxer yangu niiweke mfukoni mwa suruali
yangu huku tishet yangu nikiwa nimeishika mkononi huku nikitaka kuivaa
“Dogo unakwenda wapi?”
“Ehee”
”Hujasikia…! Unakwenda wapi?”
“Kununua vitafunio vya chai”
“Dogo mbona unajifanya mjanja sana?”
Maswali ya jamaa yakazidi kunichanganya akili na kunizidisia presha ambayo sikuelewa kama inapanda au inashuka.
“Mjanja wa nini brother?”
“Huendi kununua vitafunio ila sema ninakwenda kununua vitafunwa kwani vitafunio ni hayo meno yako”
“Sawa bro nimekuelewa”
“Ehee kwanza hujaniambia wewe ni nani? Nakuona upo upo tu humu ndani?”
“Mimi ninaitwa Eddy”
“Yuko wapi Mery?”
Nkaanza
kufikiria cha kumjibu huku maswali mengine nikijiuliza mwenyewe na
kujijibu mwenyewe ndani ya moyo wangu hadi nikapata muafaka wa nijibu
nini
“Amelazwa kwenye hospitali ya shule”
“Lini?”
“Leo asubuhi”
Lengo
la kumjibu jamaa kiufasaha kila swali analo niuliza ni ili akienda
kumuangalia Madam Mery iwe nafasi ya mimi kuondoka katika nyumba hiyo
ili nikatafute hata sehemu ya kuishi nikisubiria siku zangu za
kusimamishwa masomo ziishe
“Powa dogo vaa tisheti yako unipeleke huku alipolazwa”
Sikuwa
na ujanja zaidi ya kuivaa tisheti yangu na kumalizia kuvaa viatu vyangu
na kitu kilichozidi kuniweka mpole mbele ya jamaa ni pale alipoitoa
bastola yake na kutazama kama inarisasi za kutosha kwenye magazine yake
na kuirudisha kiunoni bastola yake huku akionekena kuridhika na risasi
zilizomo.
Safari
ikaanza huku sote tukiwa kimya ila mimi nimetangulia mbele kama hatua
moja huku yeye akifwatia kwa nyuma.Akili yangu ikawa inanituma nipige
hatua za haraka haraka na kama kuna uwezekano nikimbie kwani vichochoro
vyote ninavijua katika mji huu wa Arusha
“Dogo nasikia kuna majambazi sana wamezuka kipindi cha hivi karibuni?”
“Kusema
ukweli bro mimi mwenyewe ninasikia sikia ila sina uhakika kivile.Ila ni
juzi kuna benki pale mbele ilivamiwa na pesa zote zikaibiwa”
“Dogo subiri ninunue P.K hapa dukani si utakula?”
“Ndio”
Jamaa
akaingia kwenye moja ya duka,nikamchungulia kwenye duka hilo nikamuona
yupo bize na muuza duka.Nikaanza kupiga hatua za taratibu huku nikizuga
zuga watu waliopo katika eneo hilo wasistukie kitu chochote ili nikifika
mbali na duka hilo nianze kukimbia.Kabla sijafika mbali kidogo gafla
nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma.Nikageuka na kukutana na muuza
mahindi
“Oya broo yule jamaa pale mjeda ameniambia nikuletee maindi uchague”
Nikatamani
nimtukane muuzaji wa watu ila nikaona hana kosa taratibu nikaanza
kuyatazama mahindi yaliyo chomekwa kwenye spoke za baiskeli zipatazo
kumi na kuunganishwa katika mti mmoja.Nikachagua muhindi laini laini
kwani sikuwa nimekula kitu cha aina yoyote tangu asubuhi.Jamaa akaja
hadi tulipo akatoa noti ya elfu kumi na kumpa muuza maindi na kumuambia
chenchi akae nayo
“Aisee kamanda wangu Mungu akubariki sana”
Muuza
maidi alizungumza kwa lafudhi ya kichaga huku akipiga saluti na
kumfanya jamaa acheke ila mimi sikuwa na hata hamu ya kuyakenua meno
yangu.Tukaendelea na safari ya kwenda katika hospitali ya shule ambayo
haikuwa mbali sana na shule kwani ilikuwa pia inatoa msaada wa
kuwahudumia wananchi wa kawaida tofauti na wanafunzi
Tukafika
hospitalini na tukakutana na Madam Rukia akiwa nje ya wodi ya
wagonjwa,nikamsalimia nikabaki nikiwatazama jinsi anavyo salimiana na
jamaa huku wakicheka kwa furaha na kuonekana wakifahamiana kwa muda
mrefu
“Huyo mwenzako anaendeleaje?”
“Kidogo joto lake limeshuka kwani asubuhi hali yake haikuwa nzuri kivile”
“Tatizo lake ni nini haswa?”
“Maleria alikutwa na vidudu sita ndio vimemlaza.”
“Sasa mbona umekaa huku nje?”
“Nilitoka mara moja kupunga punga hewa ila twende ukamuone”
Wakati
wote wanazungumza nilikuwa kimya nimetulia kama maji ya mtungini huku
moyoni nikifurahia jamaa aingie ndani na mimi niondoke .Jamaa na Madam
Rukia wakaanza kuingia ila jamaa akasimama na kuniangalia
“Oya dogo twende ukamuangalie mgonjwa”
“Huyu mwalifu umemtoa wapi?”
Madam
Rukia alimuuliza jamaa na kumfanya atabasamu ila kwangu nikazidi
kuogopa,cha kumshukuru Mungu jamaa hakulijibu swali la Madam Rukia kwani
tayari tulishafika ndani ya chumba alicholazwa Madam Mery.Jamaa akakaa
kitandani na kumkumbatia madam na wote kwa pamoja wakawa wanatokwa na
machozi ya furaha,sikujua kinacho waliza ni nini
Wakaachiana
huku jamaa akianza kumfuta Madam Mery machozi kwa kutumia kitambaa
chake na kunifanya roho yangu kuanza kuhisi maumivu ya wivu