Majambazi
sita wameuawa kwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za miili yao na
Jeshi la Polisi baada ya kutokea majibizano ya risasi kati ya polisi na
majambazi hao na kupatikana silaha moja aina ya AK 47 na nyingine nne
zilizotengenezwa kienyeji.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea
usiku wa Julai 8, 2017, katika mtaa wa Fumagila mashariki kata ya
Igoma wilaya ya Ngamagana mkoani Mwanza baada ya kupokea taarifa kwa
kwamba baadhi ya watu wanaofanya uhalifu katika mkoa wa Pwani wilaya ya
Kibiti na Rufiji wamekimbilia mkoani humo wakijipanga kutengeneza
vikundi vya kufanya uhalifu.
Kamanda
Msangi amesema katika ufuatiliaji walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa
mmoja ambaye katika mahojiano alikiri kuhusika na tukio la unyang'anyi
kwa kutumia silaha, kisha alitoa ushirikiano kwa askari ambapo
aliwapeleka hadi eneo la Fumagila ambapo alidai wenzake wamejificha eneo
hilo, ghafla majambazi hao walikurupuka na kuanza kuwarushia askari
polisi risasi.
Aidha,
kutokana na umahiri wa askari hao waliweza kujibu mashambulizi na
kufanikiwa kuwauwa majambazi sita huku wengine wawili wakifanikiwa
kutoroka eneo la tukio lakini polisi walifanikiwa kukamata silaha kadhaa
na vitu vingine.
Pamoja
na hayo, DCP Msangi amesema hakuna askari aliyejeruhiwa kwa risasi wala
kupoteza maisha katika tukio hilo huku akisisitiza kuwa ufuatiliaji wa
kusaka na kuwatia nguvuni waliotoroka bado unaendelea.
Shuhuda
wa tukio hilo, ambaye ni diwani wa Kata ya Kishili iliyo jirani na kata
hiyo, Sospeter Ndumi amesema kurushiana risasi baina ya watu hao na
polisi kulianza usiku wa manane hadi majira ya jana asubuhi.
Amesema
katika majibizano hayo polisi walifanikiwa kuwaua watu hao na kukamata
silaha mbalimbali za kivita walizokuwa wanazitumia.
Katika
mtaa huo huo ndipo lilipotokea tukio la Desemba 3 mwaka jana ambapo
polisi waliwakamata watoto 11 wenye umri unaokadiriwa kuwa na miaka sita
hadi 14 baada ya kuizingira nyumba moja kwa lengo la kuwakamata watu
waliowahisi kuwa majambazi.
Mmoja
kati ya watu watatu waliokutwa kwenye nyumba hiyo alikimbia baada ya
kuwarushia polisi bumu la mkono, kabla ya polisi kuwadhibiti waliosalia
kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa huo.
Kadhalika
katika tukio hilo, watu watatu waliosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa
na bunduki mbili aina ya SMG na AK47, magazine saba, bastola moja na
risasi 183 vilikamatwa na polisi.
Baada ya polisi kuondoka katika eneo hilo, wananchi waliiteketeza nyumba hiyo kwa moto.
0 comments:
Chapisha Maoni