test

Jumatano, 31 Mei 2017

Diamond na Ali Kiba washindwa kurekodi wimbo wa Serengeti Boys



 Mwenyekiti wa kamati ya kuhamisha kuichangia timu ya taifa ya vijana ya umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys Charles Hilary amesema wanamuziki nguli nchini wa Bongo Flava Naseb Abdul maarufu kama Diamond na Ali Kiba wameshindwa kutunga wimbo wa kuhamasisha mashabiki wa soka nchini kuichangia timu hiyo.
Hilary amesema hayo katika mahojiano maalumu na TBC ambapo ameeleza kwamba walitarajia ushiriki wao wa moja kwa moja lakini muda mwingi wanamuziki hao waliwakilishwa na mameneja wao.
Wasanii hao  ni miongoni mwa wajumbe walioteuliwa kuwa kwenye kamati ya uhamasishaji iliyoteuliwa ma waziri wa Habari,utamaduni Sanaa na  michezo DKT. Harrison mwakyembe.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni