Waziri Maghembe amewataka watumishi
wa Mapori ya Burigi, Biharamulo na Kimisi mkoani Kagera kutoruhusu tena
mifugo kuingia ndani ya mapori hayo
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amewataka watumishi wa Mapori ya Burigi, Biharamulo na Kimisi yaliyopo Mkoani Kagera kutoruhusu tena mifugo kuingia ndani ya mapori hayo na kuutaka uongozi wa mkoa kuhakikisha minada ya mifugo iliyokamatwa inaendeshwa kwa uwazi.
Waziri Maghembe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa mapori hayo pamoja na uongozi wa Mkoa wa Kagera katika ziara yake ya siku moja Wilayani Biharamulo.
Aidha amesema wizara yake ina mipango ya kutoa mafunzo zaidi kukabiliana na ujangili pamoja na watu wanaoingiza mifugo ndani ya maeneo hayo ya hifadhi.
Profesa Maghembe ameutaka uongozi wa Mkoa wa Kagera kusimamia kikamilifu minada ya mifugo iliyokamatwa wakati wa oparesheni.
Kadhalika amesema utaratibu wa doria katika mapori hayo tengefu utaendelea kama kawaida kwa kutumia ndege ndogo pamoja na ziLe zisizokuwa na rubani.
0 comments:
Chapisha Maoni