Rais
wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye pia ni
Mbunge wa Singida Mashariki amefunguka kwa kusema chama ACT-Wazalendo
kinatumiwa katika kuvunja upinzani uliopo nchini na serikali ya CCM.
Lissu
amebainisha madai hayo baada ya Rais Magufuli kumteua aliyekuwa
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro aliyeapishwa jana katika viunga vya Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
"Hao
siyo wapinzani hawajawahi kuwa wapinzani, walianzishwa kwa kazi maalumu
ya kuua upinzani imeshindikana sasa wanapewa zawadi. ACT na Anna
Mghwira walikuwa wakabariane na Lowassa nasiyo CCM walipata kura chache
hata laki moja hazikufika. Huu ukuu wa Mkoa ni zawadi tu, Ukatibu Mkuu
wa Kitila Mkumbo ni zawadi tu wanawazawadia watu wao hawa siyo
wapinzani" alisema Lissu.
Aidha,
Lissu amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijawahi kuwa na shida
ya aina yeyote na viongozi wa ACT bali shida yao kubwa ni CHADEMA na
CUF.
"Serikali
ya Chama cha Mapinduzi (CCM), haijawahi kuwa na shida na ACT wala
Kitila Mkumbo, haijawahi kuwa na shida na Anna Mghwira na hao wanaojiita
wapinzani wote, shida yao kubwa ni CHADEMA na CUF ndiyo wapinzani
wengine wote hawa ni wana CCM" alisisitiza Lissu.
Pamoja
na hayo, Lissu amesema haitoweza kuja kutokea kwa Rais Magufuli kuja
kumteua yeye kwa nafasi yeyote na endapo itatokea hivyo basi atamtaka
kwanza abadilishe katiba mpya ili waweze kutengeza nchi mpya.
0 comments:
Chapisha Maoni