Makamu
wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amesema kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao
hawataki kufanya kazi na kusubiri chakula kutoka Serikalini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana
ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya
Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo
mjini Musoma.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Serikali itapeleka
chakula kwa wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka
kwa ukame au kwa maafa mengine na sio kwa wananchi wanaokaa vijiweni
mchana kutwa bila kufanya kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa
Serikali.
Amewahimiza
wananchi kote nchini kuendelea kufanya kwa bidii ikiwemo shughuli za
kilimo na pindi wanapovuka wajiwekee akiba na waache tabia ya kuuza
mazao yote wanayovuka ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula
kwenye familia zao.
Makamu
wa Rais pia amewataka viongozi wa mkoa wa Mara washirikiane na wananchi
katika kuwaelemisha mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi
ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.
Kuhusu
tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama
kufanya misako ya hali na mali katika kupambana na tatizo hilo ambalo
limechangia kupunguza samaki katika maeneo mbalimbali nchini.
Ametoa
mfano kwa mkoa wa Mara kuwa ulikuwa na viwanda Vinne vya kuchakata
samaki lakini kutokana na shughuli za uvuvi haramu na wa kutumia sumu
umepelekea viwanda Vitatu kukosa malighafi hiyo na kusitisha uzalishaji.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema jambo hilo ni baya kwa sababu
limeikosesha Serikali mapato na kusababisha wananchi wakose ajira kutoka
kwenye viwanda hivyo jitihada za makusudi lazima zifanyike katika
kukomesha uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika Ziwa
Victoria.
Aidha,
Makamu wa Rais ameeleza kufurahishwa na kukamilika kwa mradi mkubwa wa
maji wa Musoma ambao umetekelezwa na Serikali ya Tanzania na Serikali ya
Ufaransa na kusema kuwa mradi huo utaondoa tatizo la upatikanaji wa
maji safi na salama kwa wananchi wa wilaya ya Musoma.
Amewataka
wananchi wa Manispaa ya Musoma kuulinda na kuutunza mradi huo ili uweze
kudumu kwa miaka mingi kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Manispaa
hiyo.
Naye,
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dakta Charles Mlingwa amewahimiza wananchi wa mkoa
wa Mara kuweka itikadi zao kando na washirikiane katika utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Musoma – Mara
7-June-2017 .
0 comments:
Chapisha Maoni