Chadema
imelaani vikali kauli ya Rais wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi
aliyesema kuwa kama siyo matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John
Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote.
Kiongozi
huyo wa awamu ya pili ambaye alikuwa akizungumza kwenye swala ya Eid El
Fitri alidai pia laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa
uongozi wa urais, amengemshauri Rais Magufuli awe Rais wa Tanzania wa
siku zote.
Akizungumzia
kauli hiyo katika makao makuu ya Chadema yaliyopo Kinondoni, leo
(Alhamisi) Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee, Roderick Lutembeka amesema
matamshi hayo yanapaswa kukemewa kwa vile yanaashiria kulipeleka Taifa
kuandaa viongozi watakopuuza Katiba ya nchi.
“Sisi
wazee wa Chadema kwa kutambua madhara ya kauli kama hizi tumeamua
tusikae kimya kwani kauli hiyo inakiuka Katiba ya nchi inayoweza
kulitumbukiza Taifa katika machafuko kama ambavyo imetokea kwa nchi
jirani zilizopuuza uvunjifu wa katiba,” amesema.
Amewataka
Watanzania kwa ujumla kujitokeza na kupinga kauli za namna hiyo ambazo
alisema zinajaribu kuwaandaa wananchi kisaikolojia ili kuwa na viongozi
watakaopindisha Katiba katika siku za baadaye.
==>Msikilize hapo chini akiongea
0 comments:
Chapisha Maoni