Mwanyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelitaka
jeshi la polisi nchini kutowafunga midomo na kusema kitendo cha jeshi
hilo kuwafukuza waandishi wa habari wakati wakifanya kazi yao si sawa.
Freeman
Mbowe amesema hayo leo Alhamisi baada ya jeshi la polisi kuwafukuza
waandishi wa habari ambao walikuwa wakifuatilia tukio la kuwasili kwa
Mhe. Edward Lowassa Makao Makuu ya Polisi ambapo leo alikwenda kuitika
wito wa jeshi hilo baada ya juzi kutoa maelezo na kutakiwa kufika leo
tena.
Mhe
Edward Lowassa alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai
(DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi siku ya Jumanne
tarehe 27 kufuatia kauli zake alizozitoa ambazo zinasemakana kuwa ni
uchohezi
Lowassa
juzi alifika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kutoa maelezo yake kwa
muda wa masaa manne, kisha baada ya hapo alijidhamini mwenyewe na
kutakiwa kufika siku ya Alhamisi ya tarehe 29 Julai 2017 ambapo amefika
na kuambiwa uchunguzi wa jambo lake haujakamilika hivyo arudi tena
tarehe 13 Julai 2017.
==>Msikilize hapo chini akiongea
0 comments:
Chapisha Maoni