MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Nusu
saa zima likakatiaza, Shamsa mapigo yake ya moyo hayakuweza kurudi,
kila daktari aliye kuwemo kwenye chumba hicho akakata tamaa. Hadi
daktari mkuu Bi. Sharmaa.
“Dokta mgonjwa ameshafariki huyu”
Daktari msaidizi alizungumza kwa msisitizo.
“Muandaeni kwa ajili ya kumpeleka Mochwari”
Bi
Sharmaa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Kwa kipindi cha
miaka ishirini katika kazi yake ya udaktari hakuna siku ambayo aliweza
kuguswa na kifo cha mgonjwa, kama kifo cha Shamsa. Hakuhitaji kulia
mbele za watu, akafungua mlango na kutoka
“Dokta hali ya mgonjwa vipi?”
Madam
Mery alimuuliza Bi Sharmaa, huku akimtazama mwana mama huyo. Bi
Sharmaa, akamtazama madam Mery kwa macho yaliyo jaa huruma, mbaya zaidi
machozi akajikuta yakimwagika. Kitu kilichomfanya madam Mery kuhisi hali
ya hatari imetoke
“SHAMSA AMEFARIKI DUNIA. SAMAHANI KWA HILO”
Bi Sharmaa alizungumza na kuondoka na kumuacha Madam Mery akiwa mdomo wazi asijue afanye nini.
ENDELEA
Taratibu
Madam Mery akajikuta akitafuta sehemu na kukaa, mwili mzima ulimuishia
nguvu, kifo cha Shamsa ni kifo kilicho mstaajabisha kwa maana ni jana
mchana alikuwa naye kutwa nzima.
‘Sasa nitafanyaje mimi?’
Ni swali alilio jiuliza madam Mery akiendelea kububujikwa na machozi usoni mwake
***
Safari
ya kufika katika nyumba ya raisi Praygod haikuchukua muda sana, kila
mtu ndani ya gari hakuzungumza chochote, kila mtu kichwani mwake aliwaza
chake. Rahab akaonekana kustuka baada ya kuukuta mlango wa kuingilia
ukiwa na tofauti kidogo na jinsi walivyo uacha.
“Vipi”
Raisi Praygod aliuliza baada ya kuona mabadiliko ya sura ya Rahab.
“Kuna tatizo ndani, nisubirini nje”
Rahab
alizungumza kwa kujiamini na kuwaacha Sa Yoo na Raisi Praygod kusimama.
Eddy akaarudi hatua mbili nyuma kutoka katika sehemu alipo simama na
kutazama upande wa pili wa nyumba ambapo aliweza kuona mlango wa sehemu
hiyo ya nyuma ukiwa wazi.
Bila
kumueleza mtu yoyote kitu, akaanza kuelekea kwenye mlango huo kwa
tahadhari kubwa. Kitendo cha kufika karibu na mlango huo, kufumba na
kufumbua, akastukia gongo zito likitua kifuani mwake na kumuangusha
chini. Akiwa amelala chini akastukia mtu akiwa amesimama mbele yake, cha
kushangaza Eddy akajikuta akiishiwa nguvu na kubaki akimtumbulia macho
mtu huyo.
***
Phidaya baada ya kuingia ndani ya Taksi moja kwa moja akamuomba dereva
taksi ampeleke nyumbani kwa raisi Praygod. Hawakuchukua muda mwingi
wakafanikiwa kufika nyumbani kwa raisi Praygod. Hali ya ukimya ikaanza
kumpa wasiwasi mwingi Phidaya, kwani tangu akae wiki kadhaa kwenye
nyumba hiyo hajawahi kuona ukimya wa namna hiyo. Hapakuwa na sauti ya Tv
au redio kama ilivyo zoeleka. Kwa haraka akaangaza macho yake huku na
kule, hakuliona gari la Raisi Praygod analo litumia.
‘Wamekwenda wapi?’
Ni
swali ambalo Phidaya alijiuliza baada ya kuufungua mlango, huku akiwa
na mashaka moyoni mwake. Akaanza kuingia ndani akiwa katika mwendo wa
tahadari, kama alivyo fikiria kichwani mwake kweli hakukuta mtu wa aina
yoyote ndani humo.
Akiwa
katika kushangaa shangaa, akastukia mlango ukifunguliwa, akageuka kwa
haraka na kumkuta dereva taksi aliye mleta eneo hilo akiwa amesimama,
uso wake ukionekana ukiwa katika hali ya hasira tofauti na jinsi alivyo
muacha ndani ya gari.
“Unanichelewesha dada nahitaji pesa yangu”
Dereva
taksi alizungumza kwa msisitizo mkubwa, ulio mfanya Phidaya kuingiwa na
hofu kidogo. Dereva huyo anaye onekana ni mzee wa makamu kiasi mwenye
ndevu nyingi usono mwake, zilizo fungamana kama ndevu za gaidi mmoja
aliye kuwaa maarufu duniani kwa usumbufu wake, Osama Bin Laden. Mavazi
aliyo yavaa yalidhihirisha kwamba ni mtu wa sala na asiye penda ujinga
katika mambo yake.
“Ku….kuu kuna ndugu zangu na…wasu….biri waniletee pesa”
“Hadi saa ngapi, nimekaa hapo nje na kusubiria au unaniletea utapeli wako si ndio?”
Mzee
huyo alizidi kumjia juu Phidaya na kumfanya azidi kuchanganyikiwa kwa
woga. Dereva huyo akazidi kuikunja sura yake huku akianza kumsogelea
taratibu Phidaya, ambaye naye alianza kurudi nyuma kwa woga. Macho ya
mzee huyo yakaanza kumtazama Phidaya kuanzia juu hadi chini, taratibu
macho ya mzeee huyo yakaanza kumlegea na kuingia na tamaa ya mapenzi,
alipo dhibitisha kwamba hakuna mtu mwengine yoyote ndani ya nyumba hiyo
dhaidi ya wao wawili tu.
“Naomba pesa yanguuu”
Mzee
huyo alizungumza huku macho yakimlegea, sehemu ya mbele ya suruali yake
maeneo ya zipu, ikaanza kutuna taratibu, kitu kilicho mpa Phidaya
ufafanuzi wa kwanini mzee huyo aliingia humo ndani, ingali alisha
mueleza amsubirie kwenye gari. Phidaya katika kurudi rudi kwake nyuma
akafanikiwa kufika kwenye mlango wa kutokea nje upande wa pili wa nyumba
hiyo. Mzee huyo bila hata kusita akaanza kumkimbiza Phidaya, bila ya
kujali nini hatari ya yeye kufanya hivyo.
Akilini
mwake tayari alisha tawaliwa na jini la mahaba na alicho kihitaji yeye
kwa wakati huo ni penzi la Phidaya mwanamke aliye muona ni mzuri kuliko
hata wake zake wanne alio waacha nyumbani kwake. Phidaya akafanikiwa
kutoka nje na kumuacha mzee huyo hatua kadhaa, kwa haraka Phidaya
akatazama tazama eneo la nyuma ya nyumba hiyo, kulipo hifadhiwa, baadhi
ya vitu vilivyo malizia ujenzi wa nyumba hiyo.
Kwa
haraka Phidaya akaokota moja ya gongo na kulishika kwa umakini kitendo
cha mzee huyo kutokeza sura yake kwenye kona aliyo jibanza Phidaya,
gongo zito likatua kwenye pua yake, kitendo kilicho mfanya mzee huyo
kutoa ukelele mkali wa maumivu. Phidaya akamuongeza mzee huyo gongo
jengine la mgongo na kumfanya mzee huyo kutoka baru, moja kwa moja
akaelekea kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo akiyasikiulizia maumivu
makali ya mgongo aliyo yapata.
Phidaya
akashusha pumzi nyingi huku taratibu akikaa chini, machozi yakimwagika
usoni mwake. Kwa msongamano wa mawazo na kuchoka, usingizi ukaanza
kumnyemelea Phidaya taratibu na kujikuta akipitiwa na usingizi akiwa
amekaa eneo hilo huku gongo lake akiwa amelishika mkononi. Haukupita
muda mlio wa gari ukamstua na kujikuta akikurupuka na kusimama huku
mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi.
Akajibanza
tena kwenye kona yake, kitendo cha kuchungulia, akamuona mwanaume aliye
kuwa akimkimbiaza amesimama katika eneo la nyumba hiyo, kwa bahati
mbaya Phidaya katika kurudi nyuma akajikuta akikanyaga kipande cha bati,
kilicho toa ukelele ulio mstua mtu aliye kuwa akimkimbiza. Phidaya
mwili mzima ukamtetemeka baada ya kumuona mtu huyo akitazama eneo hilo
kwa umakini na kuanza kutembea hatua za tahadari akimfwata.
Phidaya
huku akiwa anatetemeka mwili mzima akalishika vizuri gongo lake, kwa
mikono miwili, mtu huyo aliye hisi amumuona akazidi kumfwata , kabla
hajaufikia mlango, Phidaya akalirusha gongo hilo lililo tua kifuani mwa
mtu huyo na kumuangusha chini. Kwa haraka Phidaya akajitokeza mbele ya
mtu huyo kwa haraka akihitaji kuliokota gongo lake. Mtu huyo alionekana
kuzubaa akimshangaa.
Phidaya
bila kupoteza muda akaliokota gongo lake, baada ya kumuona mtu huyo
akiwa anamshangaa shangaa pasipo kufanya kitu chochote. Akalivuta kwa
nguvu na kutaka kulishusha kichwani mwa mtu huyo anaye muona ni miongoni
mwa watu walio agizwa na dokta Ranjiti.
“Phidaya Stop”(Phidaya acha)
Sauti ya mwanaume huyo ikamfanya Phidaya kusita kidogo, kwani si sauti ngeni kwenye masikio yake.
“Phidaya ni mimi Eddy”
Phidaya akajikta kigugumizi kikali kikimshika, huku kikiambatana na bumbuazi kali.
“Tafadhali Phidaya ni muda mrefu nilikuwa nikikitafuta mke wangu, tafadhali usinidhuru”
Eddy
alizungumza huku taratibu akinyanyuka, akampeleka Phidaya mkono wa
kulia huku akihitaji kumshika ila Phidaya akaukataa mkono huo, kwani
sauti ndio ni ya mume wake Eddu ila sura ndio inayo mzuzua.
Phidaya akalivuta gongo lake kwa nguvu na kutaka kumpiga nalo Eddy, akiamini mtu huyo anatumia sauti ya mume wake Eddy.
“PHIDAYAAAA”
Sauti
ya Rahab ndio iliyo mfanya Phidaya kusita kwa mara nyingine, huku sura
yake akimtazama Rahab aliye tokea kwenye mlango uliopo eneo hilo. Sauti
ya Rahab iliwastua Sa Yoo na raisi Praygod na wote kwa pamoja
wakakimbilia eneo la nyuma ya nyumba hiyo inapo tokea sauti hiyo.
Wote wakamkuta Phidaya akiwa amelishikilia gongo lake kwa mikono miwili huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasira.
“Madam”
Sa Yoo aliita huku macho yakiwa yamemtoka.
“Madam ni mimi Sa Yoo”
Sa Yoo alizungumza huku akimsogelea Phidaya. Kila mtu alikaa kimya akiwatazama Phidaya na Sa Yoo
“Upo katika mikono salama, madam”
“Shamsa yupo wapi?”
Phidaya alizungumza akiwa bado hajalishusha gongo lake analo taka kumpiga nalo Eddy asiye muamini kama ni Eddy kweli.
“Shasma nimemuacha hotelini, naamini tukitoka hapa tutakwenda kumuona”
Kwa
maneno ya Sa Yoo, kidogo Phidaya akaanza kiliteremsha gongo lake chini,
Sa Yoo akalichukua gongo hilo na kulitupa pembeni kisha akakumbatiana
na Phidaya, wote wakajikuta wakimwagikwa na machozi.
“Nahitaji kuonana na Shamsa anidhibitishie kwamba huyu ni Eddy au laa”
“Sawa
hakuna tatizo ila ninaomba uamini kwamba huyo ndio mumeo. Ila hiyo ni
sura bandia aliyo ivaa alifanyiwa oparesheni akiwa Japani”
“Sitaki kuliamini hilo nahitaji kuonana na Shamsa mwanangu kwanza”
Hapakuwa
na mtu aliye weza kubisha hilo. Wala Eddy hakuzungumza chochote zaidi
ya moyoni mwake kujawa na furaha ya kuiweza kumuona mke wake. Hapakuwa
na haja ya kuingia ndani wote wakaingia kwenye gari. Safari ya hotelini
ikaanza, kwa mara kadhaa, Phidaya aligeuka nyuma kumtazama Eddy, ila
moyoni mwake hakuhitaji kukubali kwamba huyo ni mumewe.
Wakafika hotelini na wote wakashuka, moja kwa moja wakelekea kwenye
chumba ambacho analala Shamsa na Sa Yoo. Wakaingia kwenye chumba ila
hawakumkuta Shamsa.
“Anaweza kuwa katika chumba cha madam Mery”
Sa
Yoo alizungumza nakutoka kuelekea kwenye chumba hicho ila hakumkuta pia
madama Mery, hakuwa na mashaka yoyote akaamini kwamba Shamsa na madama
Mery wanaweza kuwa pamoja. Akatoka kwenye chumba hicho na kuanza
kutembea kwa hatua za haraka kurudi katika chumba alipo waacha wezake,
kabla hajakifikia akakutana na muhudumu, akamsimamisha.
“Samahani dada, kuna mwenzangu yule mwenye asili ya kiarabu arabu umemuona wapi?”
“Wa chumba kipi?”
“Ninalala naye chumba hicho hapo”
Sa
Yoo akamuonyesha muhudumu huyo kwa kutumia mkono, muhudumnu akageuka
nyuma, akakitazama chumba anacho onyeshwa na Sa Yoo, akashusha pumzi
nyingi kisha akamgeukia Sa Yoo na kumtazama usoni.
“Ulikuwa wapi kwani?”
“Kivipi dada sijakuelewa?”
“Msichana wa chumba hicho amewahishwa hospitalini kwa maana hali yake asubuhi ilikuwa mbaya”
“What…….!!!”
“Ndio”
Sa
Yoo akaonekana kuchanganyikiwa kwa taarifa hiyo kwa haraka akaelekea
kwenye chumba alicho waacha wezake, kila aliye muona akatambua kwamba
kuna tatizo ambalo limetokea. Kabla Sa Yoo hajazungumza kitu chochote
muhudumu aliye kuwa akizungumza naye akaingia, baada ya kumuona Sa Yoo
amechanganyikiwa. Akawaelekeza watu wote hali nzima ilivyo tokea na
hosputali aliyo pelekwa.
Hapakuwa na muda wa kupoteza., wakajumuika kwa pamoja muhudumu huyo na moja kwa moja wakaelekea hospitalini.
Eddy
ndio akawa mbele kwa kutembea kwa mwendo kasi kuelekea walipo elekezwa
mapokezi kulipo na chumba cha upasuaji. Jasho lilimtiririka Eddy usoni
akili na moyo wake havikuwa tayari kuweza kusikia taarifa yoyote mbaya
kuhusiana na Shamsa.
Wakamkuta Madam Mery akiwa amekaa kwenye moja ya kiti amejiinamia chini.
“Mery kuna nini kilicho tokea”
Eddy
aliuliza kwa shauku, mapigo ya moyo yakimuenda kasi. Madam Mery
akanyanyua kichwa chake na kumtazama Eddy. Macho yake yaliyo jaa
uwekundu, ulio sababishwa na kulia kwa muda mrefu, kulimstua kila mtu.
“Mery niambie ni nini kilicho tokeaa”
Eddy
alizungumza kwa sauti ya msisitizo wa hali ya juu, huku jasho
likiendelea kumwagika. Phidaya akamkazia macho madam Mery na kukumbua ni
miongoni mwa watu walio mtesa kipindi ana ujauzito wa marehemu mwanaye
Junio.
“Sha…msa AMEFARIKI DUNIA”
“WEWE MUONGOOOOOOOOOOOOOOOO…………….”
Phidaya
alizungumza kwa hasira na kumrukia madam Mery sehemu alipo lala na
kuanza kumshindilia mangumi akikumbukia kipindi alivyo mtesa akiwa yeye
na Eddy. Eddy akajari kumtoa Phidaya ila akashindwa na kujikuta
akisukumwa pembeni. Rahab akajaribu bahati yake ila kwa bahati mbaya
akastukia kisukusuku kizito kutoka kwa Phidaya kikitua kichwani mwake,
akayumba yumba na kuanguka chini kisha akapoteza fahamu. Huku Phidaya na
madam Mery wakiendelea kuparangana Phidaya akionekana kuwa na hasira
kali juu madam Mery
SORRY MADAM (73) (Destination of my enemies)
Walinzi
walio karibu na eneo hilo ikawabidi wasaidiane na Eddy pamoja na raisi
Praygod kuwatenganisha madam Mery na Phidaya ambao wote walionekana
kupandwa na hasira na kila mmoja aliweza kurusha makondo kwa mwenzake
kwa kadri alivyo weza kufanya hivyo.
“Munafanya nini mbele za watu hamuoni aibu?”
Raisi Praygod alizungumza kwa hasira huku akiwatazama, Phidaya na madam Mery kwa macho makali.
“Hamujui ni wapi mulipo, akili zenu hivi zina akili?”
Raisi
Praygod aliendelea kufoka kwa hasira. Sa Yoo hakuhitaji kuufwatilia
ugomvi huo zaidi ya kuendelea kumuamsha Rahab aliye lala chini kimya.
“Nesi nesi naomba msaada wenu”
Sa
Yoo alizungumza huku akimshika sketi nesi mmoja aliye simama pembeni
yake, utaratibu wa kumbeba Rahab na kumpeleka kwenye chumba cha huduma
ya kwanza, ukaanza huku Sa Yoo akifwata kwa nyuma. Eddy akamshika mkono
Phidaya na kuanza kumvuta na kumtoa katika eneo hilo.
Wakakatiza
kwenye moja ya kordo, Eddy akaona maandishi meusi yaliyo andikwa
Toilet. Kwa haraka pasipo kutazama kwa umakini kama choo hicho ni cha
kiume au ni cha kike kwa haraka akashika kitasa cha mlango huo na
kuufungua kwa nguvu na kuingia ndani huku akimvutia Phidaya kwa ndani.
“Unanivutia nini?”
Phidaya aliuliza kwa hasira huku ajitoa mkono wake kwenye kiganja cha Eddy.
“Ni ujinga gani unao ufanya mbele za watu, hujua kwamba hapa ni hospitalini?”
“Unaniuliza hivyo wewe kama nani?”
Phidaya alizungumza huku akimsukuma Eddy kwa nyuma.
“Hujua unazungumza na nani?”
“Eheeee, hivi nilivyo kuambia ya kwamba siwezi kukuamini hadi Shamsa anidhibitishie unahisi ninakutania?”
“Please
Phidaya, amini ninalo kuambia hii sura ninayo itumia hapa sio sura
yangu halisi, nimeivaa kutokana na usalama wangu kuwa mdogo”
“Vua niione sura yako halisi”
“Nikiivua hii sura itanisababishia maumivu makali sana”
“Nimekuambia uivue”
Eddy
akashusha pumzi nyingi huku akimtazama Phidaya machoni aliye chacharuka
kwa hasira kali ambayo anayo. Kwa bahati nzuri vyoo walivyo ingia,
havitumiki kutokana na kufanyiwa matengenezo madogo madogo.
Kutokana
na upendo mwingi alio kuwa nao, taratibu Eddy akajikuta akigeukia
kwenye kioo, kilichopo humo ndani. Kwa kutumia mkono wake wa kushoto,
akaanza kuibabadua sura hiyo, japo imeshikana sana na ngozi yake halisi,
lakini hakujali. Kila jinsi alivyo endelea kuivua sura hiyo ndivyo
jinsi Phidaya alivyo jikuta akipatwa na mshangao mkubwa. Eddy akaendelea
kugugumia kwa maumivu makali hadi akamaliza kuivua sura hiyo, huku
machozi yakimlenga lenga kwa maumivu makali.
“Je umenikumbuka mke wangu”
Eddy
alizungumza kwa sauti ya unyonge machozzi yakiendelea kumwagika usoni
mwake. Phidaya bila hiyana akaitanua mikono yake yote miwili na
kumkumbatia Eddy kwa nguvu, huku naye machozi yekiendelea kumwagika kwa
uchungu.
***
Ubaridi mkali unao patika kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, ukaanza
kupenya taratibu kwenye mwili wa Shamsa. Taratibu vidole vya mguu wake
wa kushoto vikaanza kutingishika. Ubaridi huo ambao ni mkali sana na si
rahisi kwa mwili wa mwanadamu kuweza kuustahimili. Taratibu ufahamu
ukaanza kumrudia, akayafumbua macho yake kutazama ni wapi alipo, ila
giza nene, lilitawala kwenye macho yake kitendo kilicho mfanya anyanyuke
taratibu kwenye kitanda maalumu cha kuhifadhia maiti alicho lazwa.
“Nipo wapi?”
Shamsa
alijiuliza huku akilitazama shuka alilo funikiwa kuanzia miguuni hadi
sehemu ya kuiuno. Akaendelea kutazama sehemu hiyo yenye giza ila hakuona
kitu cha aina yoyote. Taratibu akashusha miguu yake chini na kukanyaga
vizuri. Akasimama, ila ubaridi wa chumba hicho ukaendelea kumtesa mwili
wake wake. Akaanza kutembea kutafuta sehemu anayo weza kutokea. Kwa
bahati mbaya akajigonga kwenye moja ya kitanda, ikambidi kupapasa papasa
juu ya kitanda hicho na kugusa mwili wa mwanadamu, kitu kilicho anza
kumpa mashaka makubwa Shamsa.
“Nipo wapi Mungu wangu?”
Shamsa
alizungumza huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana. Kwa woga Shamsa
akaanza kupiga makelele ambayo si rahisi kutoka nje ya chumba hicho
kilicho tengwa mbali kidogo na eneo la hospitali
***
Mpango wa kuanza kumtafuta Eddy karibu dunia nzima ukaanza, ukiwa chini
ya John aliye kuwa rafiki wa karibu sana na Eddy kipindi walipo kuwa
wakisoma mkoani Arusha. Dokta Ranjiti naye hakuwa mbali na kuufwatilia
mpango huo. Kila kona ya dunia wanachama wa D.F.E walijulishwa juu ya
msako huo. Picha ya Eddy iliswambazwa kwa siri sana kupitia mtandao wao
ambao si rahisi kwa mtu yoyote nje ya uwanachama kuweza kuipata picha
hiyo.
“Baba unatazama nini?”
Manka
alimuuliza Raisi Godwin baada ya kumkuta akiwa ameishikilia simu yake
kwa umakini akionekana kuna kitu anacho kitazama. Raisi Praygod
akashusha pumzi nyingi huku akimtazama Manka usoni, taratibu Manka akaka
kwenye kiti cha pembeni na kusubiria jibu kutoka kwa baba yake. Mzee
Godwin akamsogezea simu Manka akaichukua kwenye meza na kutazama kitu
alicho kuwa akikitazama baba yake.
Manka
macho yakamtoka, baaada ya kuiona Picha ya Eddy huku kukiwa na
maandishi makubwa chini yake yaliyo andikwa MOST WANTED. Taratibu Manka
akashusha pumzi na kuiweka simu hiyo mezani.
“Eddy bado anaishi?”
“Hilo ndilo jibu na wala si swali”
“Sasa baba itakuwaje?”
Mzee
Godwin akabaki kimya asijue ni nini cha amjibu Manka. Akakumbuka
usumbufu mkubwa ambao aliupata kutoka kwa Eddy kipindi cha nyuma.
‘Atakuwa wapi huyu mwa idhaya?’
Mzee Godwin alijiuliza swali ambalo hakupata jibu lake kwa haraka.
“Baba si nakuuliza itakuwaje, kwa maana mimi natambua labda Eddy amefariki?”
“Kwa sasa jibu lililopo ni lazima Eddy afariki. Zungumza na Anna, Halima, Agnes na Fetty, waambie warudi kazini sasa hivi”
“Sawa baba, nitumie hiyo picha kwenye simu yangu”
“Sawa”
Rahab
akanyanyuka huku akiitoa simu yake mkononi na kuanza kutuma mesiji wa
wezake na kuwaomba waweze kukutana naye kwenye moja ya nyumba yeke mbezi
beach. Manka akaingia kwenye gari na safari ya kueleka kwenye nyumba
yake hiyo ikaanza. Haikuchukua muda mwingi akafika kwenye jumba lake
lenye ulinzi mkali, akakuta magari ya wezake wote wanne yakiwa kwenye
moja ya maegesho maalumu. Kwa haraka akashuak kwenye gari na kuanza
kutembea kueleka ndani.
“Nashukuru kwa kuweza kufika, samahani kwa kuwasumbua jamani”
“Bila samahani”
Agnes alijibu huku akisimama na kumpa mkono wa salamu Manka. Manka akawapa walio salia kisha akakaa kwenye moja ya sofa.
“Jamani
kunakazi baba ameniomba kuweza tuifanye kwa pamoja. Ni kazi rahisi ila
si rahisi kama vile tutakavyo iona kwa maana mtu tunaye kwenda
kukabiliana naye ni hatari zaidi ya jeshi la watu mia”
“Mmmmm”
Fetty akaguna huku akishusha pumzi nyingi, akimtazama Manka usoni.
“Ni mtu wa aina gani?”
“Kwenye hii picha hapa”
Manka akamkabidhi Agnes simu akawa wa kwanza kuitazama picha ya Eddy. Kila mmoja akaitazama picha hiyo kwa umakini.
“Naamini
hiyo sura si ngeni sana kwenye macho yenu. Huyu alikuwa ni waziri wa
ulinzi kwenye serikali ya raisi aliye pita. Pia ni adui namba moja wa
baba”
“Uadui wao ni waaina gani?”
Halima aliuliza swali lililo mfanya Manka kukaa kimya kwa muda akitafakari ni nini atazungumza.
“Juu
ya huo uadui mimi sifahamu, ila kila kitu anajua mzee, na kazi iliyopo
mbele yetu ni kuhakikisha tunamtia mikononi mwetu au kumuangamiza
kabisa. Kwa maana pasipo kuweza kufanya hivyo uongozi wa mzee upo
hatarini kuanguka”
“Usijali jioni ya leo tunaanza mazoezi”
“Kabla ya kuanza mazoezi tungeweza kufahamu huyo jamaa anaitwa nani na yupo wapi kwa sasa”
“Jina lake anaitwa Eddy. Kwa sasa hatufahamu ni wapi alipo, ila kazi yetu ni kama nilivyo waeleza.”
“Sawa tumekuelewa”
Agnes
alijibu, huku akinyanyuka, wakaagana na kila mmoja akaendelea na
majukumu yake ya kikazi kwenye serikali ya raisi Godwin inayokwenda
kubadilika na kuwa serikali ya kifalme.
***
Hisia za mapenzi zikazidi kupanda kati yao, mikono ya Eddy ikawa na
kazi ya kupita kila kona ya mwili wa Phidaya. Kwa nguvu alizo nazo
akamnyanyua na kumkalisha kwenye sehemu maalumu ya kunawia mikono.
Hapakuwa na mtu aliye kuwa na kipingamizi cha kumpatia mwenzake denda la
kutosha.
Kwa
haraka Phidaya akaanza kuufungua mkanda wa suruali ya Eddy, hakuishia
hapo akafungua na zipu ya suruali hiyo na kiganja chake akakiingiza
sehemu lilipo tango lililo simama kidedea.
Viganga vya Eddy vikawa na kazi ya kuyaminya minya mziwa ya Phidaya yaliyo simama vizuri.
“Eddy tizama nyuma yakoooo”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya juu huku macho yakimtoka huku kiganja chake akikitoa sehemu lilipo tango la Eddy
0 comments:
Chapisha Maoni