Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
anatarajiwa kufungua Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam maarufu kama Sababsaba Julai Mosi mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Rais atafanya ufunguzi
huo katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya
Kilwa Jijini Dar es Slaam.
Waziri
Mwijage ameeleza katika taarifa hiyo kuwa lengo la maonesho ni kutoa
fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, pamoja na taasisi
mbalimbali kutangaza biashara na huduma, kutoa fursa kwa
wafanyabisashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora
wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza mitandao ya
mawasiliano baina yao ambayo itasaidia kukuza biashara na kufikia
malengo waliyojiwekeka na pia kutoa fursa ya kuuza bidhaa.
“Maonesho
haya yanabeba kauli mbiu isemayo Ukuzaji wa Biasha kwa Maendeleo ya
Viwanda, inanalenga kutumia Maonesho haya kama jukwaa la kutangaza
biashara na huduma mbalimbali kwa ajili ya ukuzaji wa sekta ya viwanda,
ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaweka mkazo mkubwa katika
kuendeleza uchumi wa viwada hapa nchini,” alisema taarifa ya Waziri.
Aidha
Maonesho ya mwaka huu yatatoa fursa kwa wenye viwanda vidogo, vya kati
na vikubwa kukutana na wanunuzi wa bidhaa zao na kutakuwa na kampeni
maalum ya kuhamasisha wananchi kupenda na kutumia bidhaa zinazozalishwa
hapa nchini.
“Napenda
kuwafahamisha kuwa Tan Trade kwa kushirikiana na washirika wake kwa
mara ya kwanza imeandaa Siku ya ‘Afrika Mashariki’ ambayo itaadhimishwa
tarehe 6 Julai, 2017. Lengo la siku hii ni kuimarisha biashara katika
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama inavyojulikana nchi hizi
zimejaliwa kuwa na rasilimali nyingi hali ambayo itatoa fursa nzuri
katika maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo ili kuwe na uchumi
endelevu,” ilisema taarifa hiyo.
Katika
maonesho hayo, Waziri anaeleza kuwa Tan Trade imeandaa eneo maalum
litakalojulikana kwa jina la ‘Banda la Tanzania’ kwa ajili ya
wazalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotengenzezwa ndani ya nchi na
‘Banda la Asali’ kwa ajili ya kukuza bidhaa za nyuki na pia kutakuwa na
eneo maalum la wazalishaji wa bidhaa za ngozi ambalo washiriki wake
watapata fursa ya kuonesha bidhaa bora za ngozi kwa ajili ya kuvutia
wananchi wengi kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Katika
kuimarisha huhusiano wa kibishara na kuwakutanisha wafanyabiashara wa
Kitanzania na wenzao kutoka nje ya nchi, kutakuwa na banda maalum kwa
ajili ya mikutano ya kibiashara yaani Business to Business (B2B) na pia
banda maalum litakalotumika kwa utoaji wa mafunzo ya kibiashara.
Hadi
sasa washiriki zaidi ya 2500 kutoka ndani na nje ya Afrika
wamethibitisha kushiriki Maonesho ya mwaka huu. Nchi zitakazoshiriki ni
Burundi, China, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Misri,
Ujerumani, Ghana, India, Indonesia, Iran, Italia, Japan, Kenya, Malawi
na Mauritius.
Nchi
zingine ni pamoja na Morocco, Msumbiji, Namibia, Pakistani, Rwanda,
Singapore, Afrika Kusini, Sudani Kusini, Syria, Uturuki, Umoja wa Falme
za Kiarabu (UAE), Uganda, Marekani, Uingereza na Vietnam.
0 comments:
Chapisha Maoni