Rais
wa Urusi, Vladimir Putin ametahadharisha kuwa hakuna atakasalia kama
itatokea vita kamili ya mgogoro wa kinyuklia kati ya nchi hiyo na
Marekani.
Putin
ameyasema hayo katika mahojiano na muongozaji wa filamu wa Marekani,
Oliver Stone alipotaka kupata mtazamo wake kuhusu mgogoro kati ya
mataifa hayo makubwa na yenye nguvu.
Aidha,
Rais huyo wa Urusi alipoulizwa kama kuna matumaini yoyote ya kumalizika
kwa mgogoro huo alijibu, “kuna matumaini siku zote. Hadi watakapokuwa
tayari kutupeleka makaburini na kutuzika.”
Katika hatua nyingine, Putin aliukosoa muungano wa NATO akidai kuwa ni chombo kinachotumiwa kutekeleza sera za nje za Marekani.
“Punde
tu nchi inapojiunga na muunganowa NATO, ni vigumu kukataa msukumo
kutoka Marekani na kwa bahati mbaya mfumo wowote wa silaha za Marekani
unaweza kuwekwa ndani ya nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwekwa makazi
mapya ya vikosi vya Marekani,” alisema Putin.
Alisema
kutokana na hali hiyo, Urusi inaendelea kuchukua hatua za kujihami
dhidi ya NATO na kuunda ngao za kijeshi katika mipaka yake.
Katika
hatua nyingine, Putin alijibu swali la Stone aliyetaka kupata maelezo
yake baada ya kumueleza kuwa ana taarifa za kutosha kuwa rais huyo
ameshanusurika katika majaribio makubwa matano ya kumuua.
“Ninafanya kazi yangu na maafisa usalama pia wanafanya kazi yao, na hadi sasa wanafanya kazi yenye mafanikio sana,” alijibu.
Marekani
na Urusi wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu, na sasa hali ilianza
kuonekana kutulia baada ya Donald Trump anayedaiwa kuwa rafiki wa Putin
kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani.
0 comments:
Chapisha Maoni