Ikiwa
zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha Marais
wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika
sakata la mchanga wa dhahabu (makinikia), Waziri wa Mambo ya ndani na
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wezi hao
walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostaafu ili kuzuia serikali
iache kufatilia sakata hilo.
"Wale
wenye nia mbaya wametafuta vichaka vingi sana lakini kila kichaka
wakijaribu na chenyewe kinayeyuka, walisema tutashtakiwa hivi siku hizi
mwizi naye anashtaki aliyemwibia? Kichaka hicho kikayeyuka
"Mwanzoni walikuwa wanasema mchanga tu hauna kitu lakini hili wala halihitaji shule kujua kama ni mchanga tu hauna kitu hawa watu wangekuwa wanakuja kuchukua mchanga tu kila siku. Kwa hiyo hawa watu walikuwa wanatuona kama mazuzu tu lakini Rais wetu amechukua hatua tena si kwa maneno kwa vitendo tumuunge mkono".
"Walipoona kichaka hicho kimekwama wakaanza kutaja viongozi kuwa wanahusika wakidhania hiyo itakuwa kitu cha kuzuia ili jitihada hizo zisiendelee wakaanza kutaja na viongozi wastaafu hiyo yote si kama walikuwa wanataja kuwa viongozi hao wanahusika bali walikuwa wanataka itumike kama kichaka kwamba tukitaja viongozi hao wataacha.
"Mimi niwaambie viongozi wetu hawa hawajawahi kuwa Ma- Agent wa wale wanaotuibia bali wale wanaotetea wezi ambao tumewaona ndiyo Ma- Agent wa wezi hao, na Rais akauona huo mtego akautegua sasa hivi kama ni gari lao lile basi matairi yote Rais Magufuli ameshatoa upepo, yameshalala chini" alisema Mwigulu Nchemba.

Waziri
Mwigulu aliyaongea hayo akiwa katika kijiji cha Zinzirigi katika Tarafa
ya Ndago katika mwendelezo wa ziara jimbo kwake Iramba Magharibi
kuongea na wananchi kuwaeleza alipofikia kuhusu ahadi ambazo
walikubaliana kutekeleza hasa suala la umeme kutokufika katika vijiji
vingi akieleza kuwa sababu ni mkandarasi aliyekuwepo mkoa wa Singida
aliyetolewa baada ya kushindwa kazi lakini sasa ameambiwa na watu wa
wizara ya nishati kuwa wakandarasi wawili wameshapatikana hivyo kuanzia
sasa zoezi la kuunganisha umeme vijijini utaendelea kwa kasi hasa wa REA
awamu ya Tatu.
Kuhusu
ujenzi wa zahanati alisema mpaka sasa zahanati katika vijiji vingi
alipopita zimefika hatua nzuri ya kupaua na kuwahidi kuwa pelekea mabati
na mbao na mifuko ya saruji 100 ili zahanati hizo zikamilike na kuanza
kutoa huduma mapema sana.
0 comments:
Chapisha Maoni