Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi
aliouchukua kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya
Acacia.
Ole
Sendeka ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, amesema
kuwa baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Lowassa ambaye pia
ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amempongeza Rais, hana budi
kumshukuru na kumpongeza pia kwa kufanya hivyo, na kuwaomba wabunge wote
bila kujali vyama vyao kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kusimamia
kikamilifu rasilimali za nchi.
“Nanyi
wabunge mkiwa bungeni muungeni mkono Rais wetu Magufuli anavyotetea
rasilimali za nchi ili madini yanayochimbwa yaweze kuwanufaisha
Watanzania, waweze kupata huduma zao za msingi kupitia madini hayo,” Ole
Sendeka anakaririwa na Mwananchi.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Njombe alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza jana
kwenye mazishi ya mama yake mzazi yaliyofanyika katika kijiji cha
Losokonoi wilayani Simanjiro.
Alimuomba
mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya ambaye alihudhuria mazishi hayo,
kumfikishia salamu na pongezi hizo kwa Lowassa.
Lowassa
alimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake baada ya kupokea ripoti ya
pili ya uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini yanayoshikiliwa na
Serikali katika bandari ya Dar es Salaam, yalipokuwa katika mchakato wa
kusafirishwa nje ya nchi na kampuni ya Acacia.
0 comments:
Chapisha Maoni