Mbunge
wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amezidi kukumbwa na
matukio mbalimbali baada ya jana Baraza la Taifa la Uhifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kung’oa mitambo ya umwagiliaji iliyopo
katika shamba lake na kumtoza faini kwa kuendesha kilimo eneo
lisiloruhusiwa.
NEMC
imemtoza faini ya Tsh 18 milioni Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa kosa la kuendesha shughuli za
kilimo ndani ya eneo la mita 60 kutoka kilipo chanzo cha maji.
Akizungumzi
tukio hilo jana, Mbowe ambaye yupo Dodoma ambapo vikao vya bunge la
bajeti vinaendelea alisema kuwa, zoezi zima limeendeshwa kisiasa na hii
kuthibitisha kuwa nchi yetu inaongozwa kwa chuki na husda.
Mbowe
alisema kuwa walipopewa taarifa mara ya kwanza, walikata rufaa kwa
waziri husika kwa sababu sheria inaruhusu hivyo hadi sasa walikuwa
wakisubiria majibu ya rufaa hiyo. Baada ya tukio hilo, Mbowe alieleza
kuwa atawasiliana na wanasheria wake ili kujua hatua zitakazofuata.
Zoezi
hilo la kung’oa miundombinu kwenye shamba hilo la Kilimanjaro Veggies
lilifanyika jana chini ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa na
maofisa wa NEMC.
Shamba
hilo la Mbowe liko katika Kijiji cha Nshara, Machame ambapo Januari 20
mwaka huu, DC Hai alifika shambani hapo na kusitisha shughuli zote za
kilimo kutokana na eneo hilo kuwa ndani ya chanzo cha maji.
Kwa
siku za hivi karibuni, Mbowe amekumbwa na matatizo kadhaa ambapo jengo
ilimokuwa ofisi yake ya Bilicanas na Free Media lilivunjwa na kuamriwa
kutoka, kisha siku chache baada alituhumiwa kujihusisha na dawa za
kulevya, tuhuma ambazo alikanusha.
0 comments:
Chapisha Maoni