Waziri Mkuu mstaafu, Edward
Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa nne katika Ofisi
ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa 8.15 na kuelekea nyumbani kwake.
Akizungumza
baada ya mahojiano hayo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema
Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa
6.00 mchana.
Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa
kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa
wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
"Mzee
amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23,
mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa
ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,"
amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni