Jeshi
la Polisi nchini Tanzania limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa ndani ya
Jeshi la hilo hakuna ajira zilizotangazwa, na kuwataka wananchi wote
kuwa makini na mtandao wa matapeli.
Tahadhari
hiyo imetolewa na msemaji wa jeshi hilo, Advera John Bulimba – ACP
kufuati kuibuka kwa kikundi kidogo cha matapeli wanaozunguka katika
maeneo mbalimbali hususani vijijini na kuwalaghai vijana kwamba
watawapatia ajira ndani ya Jeshi la Polisi jambo ambalo siyo la kweli.
ACP
Bulimba amesema kuwa kikundi hicho cha matapeli kilichoibuka hivi
karibuni kinazunguka maeneo mbali mbali na kuwadanganya vijana kuwa wao
ni waajiriwa wa Jeshi la Polisi na kujipatia fedha kwa udanganyifu huo.
Amesema
mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Polisi ni wa wazi na una utaratibu
maalum ambao hutangazwa kwa wananchi kwa mujibu wa taratibu za Jeshi
hilo.
Kufuatia
hali hiyo, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo
ya utapeli kuacha mara moja na endapo mtu yeyote atabainika hatua kali
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha,
Jeshi hilo limetoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa za matapeli hao
kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili
sheria iweze kuchukua mkondo wake.
0 comments:
Chapisha Maoni