Mbunge
Godbless Lema amefunguka na kutoa utabiri mwingine mpya kuwa katika
nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kila nyumba itakuwa na watu
waliomaliza shahada ya kwanza na 'masters' lakini hazitakuwa na tija
katika maisha yao na nchi kwa ujumla.
Godbless
Lema amesema hayo alipokuwa katika mahafali ya Umoja wa wanafunzi wa
elimu ya juu wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHASO)
ambapo amewataka wanafunzi hao kuwa na maadili na maono katika maisha
yao huku akisema hata katika vita ambayo nchi inapigana sasa, watu
wanaoturudisha nyuma ni wasomi ambao wameshindwa kutambua wajibu wao.
"Ambalo
mimi naliona ni vijana wenye vyeti lakini hawana 'moral authority'
nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kutoka sasa utakuta kila familia ina
degree, kila familia ina masters lakini zisizona tija. Wasomi wasio na
moral authority ni hatari kuliko wajinga wenye moral authority na hata
ukiangalia kwenye haya mapambano wanaofanya kazi yetu inakuwa ngumu ni
wasomi ambao wameshindwa kujua wajibu wao" alisema Godbless Lema
Mbali
na hilo Lema amesema wasomi wengi wa sasa ambao ni vijana wamekuwa ni
watu wasiojali mambo ya msingi, wamekuwa wakijali sana mambo yasiyokuwa
na tija katika nchi au taifa na kuikacha siasa ambayo ndiyo msingi wa
kila kitu.
"Vijana
wa sasa hamjali mnajua mambo ya mipira, yaani vijana wasomi wa nchi hii
wanajua zaidi mipira sijui 'Premier League' mimi siyajui vizuri hayo
mambo, yaani 'commitment' yenu kwenye mambo ambayo hayawezi kuleta tija
kwenye nchi imekuwa kubwa kuliko 'commitment' yenu kwenye mambo ya
siasa" alisisitiza Lema
0 comments:
Chapisha Maoni