Mchungaji wa kijiji kimoja huko zimbabwe Pastor Jonathan Mthethwa
ametafunwa vizuri na mamba watatu alipokuwa akijitutumua kutembea juu ya
maji Kama yesu katika mto MPUMALANGA
au kwa jina maarufu MTO MAMBA kutokana na wingi wa mamba katika mto huo.
Alikuwa anafanya majaribio ya imani(DEMO) aliyowafundisha waumini wake kanisani....
Shemasi aliyehojiwa anashangaa kwa nini aliliwa maana kabla alifunga na kuomba wiki nzima...
Mashuhuda wanasema alitembea ndani ya maji kama mita 30, alipotaka
kuanza kupanda ili aanze kutembea juu ya uso wa maji ndipo yalitokea
mamamba makubwa matatu na kumtafuta na kumkatata vipande huku mwili wote
ukiishia kwenye matumbo ya watafunaji hao...
Waumini Muwe makini na Wachungaji wenu, Leo kaenda yeye kesho anaweza
kuibuka mwingine TZ akawaambia kanisa zima litembee juu ya mto ruvu ile
sehemu yenye mamba na viboko wengi kama mazoezi ya Imani. Au kama
mafunzo ya vitendo baada ya kufundishwa Theory/Nadharia za kiimani
kanisani...
Imani na Akili lazima ziende sanjari na Vyote viwe mubashara Muda wote
ukikoswa kimoja utaishia kuliwa kama sio wewe basi pesa zako...
0 comments:
Chapisha Maoni